Header Ads

Hadhi ya Muziki wa Dansi Kurejea Kwa Kasi hapa Nchini

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wasanii wa Muziki wa Dansi alipokutana nao jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mungereza akizungumza wakati wa mkutano baina ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) na wasanii wa muziki wa Dansi nchini jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) Bw.Juma Ubao akizungumza wakati wa mkutano baina ya wasanii wa muziki wa Dansi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea CD yenye nyimbo ya kumsifu Mwl. Nyerere kutoka kwa mwanamuziki nguli Mzee Makassy (mwenye kofia). Katikati ni Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Hassan Msumari.
Mdau wa Muziki wa Dansi nchini Asha Baraka akichangia mada wakati wa mkutano baina ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) na wasanii wa muziki wa Dansi jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea zawadi ya CD yenye nyimbo za Bendi ya Twanga Pepeta kutoka kwa mmiliki wa Bendi hiyo Bibi. Asha Baraka mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Waziri na wasanii wa muziki wa Dansi nchini jana jijini Dar es Salaam,Kutoka kushoto ni Katibu Mtendajji wa BASATA na Rais wa Shirikisho la wasanii wa muziki nchini Bw. Ado Novemba. (wa pili kulia).

No comments

Powered by Blogger.