Header Ads

Hali Halisi Ya Zanzibar Usiku Huu


Hali ya amani na utulivu visiwani Zanzibar imeendelea kuwepo licha ya kuwepo na taarifa za kuwepo kwa vurungu visiwani humo.
Katika baadhi ya maeneo visiwani humo wananchi wameendelea na shughuli zao kama kawaida bila ya kuwepo vurungu husasani katika maeneo ya biashara.

Wakizungumza kuhusu hali ya usalama wananchi wasemema kuwa hali ya usalama imeimarishwa na hakuna vurungu kwani jeshi la polisi limejipanga kulinda raia na mali zao.

Aidha mmoja wa wafanya biashara katika eneo la darajani,Bw Rajabu Athuman Rajabu amesema kuwa,taarifa za kuwepo vurungu visiwani humo zinapotosha na baadhi ya watu wasio takia mema Zanzibar

“kwa kweli amani ipo na tunaendelea na biashara kama unavyoona watu wanapotosha na kuwafanya watu waishi kwa wasi wasi,kwani ulizi upo wa kutosha”amesema Bw Rajabu.

Kwa upande wake Bi Amina Said Salum mkazi Mazizini amesama kuwa Serikali Zanzibar inapaswa kutoa taarifa kwa wananchi wake ili wajue hali halisi ya usalama viziwani humo.

Ameongeza kuwa serikali inajukumu la kuangalia na kusikiliza maoni yanayotolewa na wananchi na kuyafanyia kazi,”serikali itusikilize na kutoa taarifa kwa wakati ili kuondoa hofu kwa watu”Bi Amina

Hata hivyo baadhi wa wananchi visiwani humo wameoneka kuwa na shauku ya kupiga kura kwa na kutoa wito kwa wananchi wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi.

Aidha katika barabara ya Amani majira ya saa mbili usiku taa za barabara hiyo zilionekana zikiwa zimewashwa na wananchi kuendelea na maisha yao ya kaiwada.

Kwa upande wa vituo vya kupigia kura vituo hivyo vimekamilisha utaratibu wa watu kuhakiki majina yao na wafanyakazi wa tume wakiwa tayari kwa kazi ya kuongoza watu kupiga kura.

Wafanya kazi katika vituo hibyo walionekana wakiwa wamepumzika baada ya kukamilisha kazi ya maandalizi,wamesema kuwa vituo hivyo vitafunguliwa mapema ili kutoa nafasi kwa wananchi kupiga kura kwa wakati.

tazama video hapo chini

No comments

Powered by Blogger.