Header Ads

Jaji Mkuu wa Zanzibar OMARY OTHMAN MAKUNGU amuapisha Dkt ALI MOHAMMED SHEIN


Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vikiingia Uwanjani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimia wageni waliohudhuria sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalah Mwinyi Khamis alipowasili katika sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume akisalimiana na Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib katika sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalah Mwinyi Khamis alipowasili katika sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi akisalimia wageni waliohudhuria sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalah Mwinyi Khamis alipowasili katika sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mwenye Joho ni Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib na Nyuma ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Christopher Olonyokie Ole Sendeka.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia wageni waliohudhuria sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalah Mwinyi Khamis alipowasili katika sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Zanzibar Omary Othman Makungu wakati wa sherehe za kumuapisha zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan ZanzibarKatikati ni Katibu wa baraza la mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi Abdulhamid Yahaya Mzee.

Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akitia saini nyaraka mara baada ya kula kiapo.

 Jaji Mkuu wa Zanzibar Omary Othman Makungu  akitia saini nyaraka mara baada ya kumuapisha Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein Katikati ni Katibu wa baraza la mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi Abdulhamid Yahaya Mzee.

 Jaji Mkuu wa Zanzibar Omary Othman Makungu akimkabidhi nyaraka Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kumuapisha Katikati ni Katibu wa baraza la mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi Abdulhamid Yahaya Mzee.

Viongozi wa Dini na Serikali wakielekea Jukwaa kuu mara baada ya kumuapisha Rais Mteule wa Zanzibar Dkr. Ali Mohamed Shein.
 
Rais Mteule wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride Mara baada ya kula kiapo.

 Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuapishwa.

Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Sheinakisalimia wageni waliohudhuria sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar.

Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza wakati wa sherehe za Kumuapisha.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa Majaliwa akimueleza jambo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimueleza jambo Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa sherehe za kumuapisha Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed.

 Ndege ikidondosha vipeperushi vya kumpongeza Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed.

Balozi wa Jamhuri ya Cuba Nchini Tanzania Jorge Luis Lopez (Mwenyeshati jeupe) akifuatilia sherehe za kumuapisha Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed.


Baaadhi ya Wananchi wakifurahia wakati wa sherehe za kumuapisha Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed.

No comments

Powered by Blogger.