Header Ads

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ( TPA ) yaipiga Jeki Hospitali ya Wilaya ya KISARAWE

Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa Vitanda 20, Magodoro 20 na Shuka 100 kwa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

Vitanda hivyo vya kisasa aina ya ‘Cardiac’, mashuka pamoja na magodoro yake vilivyokabidhiwa katika hospitali hiyo ya wilaya vina thamani ya shilingi za kitanzania milioni 13.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Mawasiliano wa TPA, Bibi Janeth Ruzangi alisema msaada huo ni sehemu ya wajibu wa Mamlaka kuisaidia jamii ya Watanzania.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt Elizabeth Oming’o hospitali hiyo ina uhaba wa vitanda 94 na mashuka 1,200.

“Hiki kilicholetwa na Mamlaka ya Bandari ni zaidi ya msaada kwani vitanda hivi ni vya kisasa na ni vya gharama sana,” alisema Dkt Oming’o.

Meneja Mawasiliano wa TPA, Bibi Janeth Ruzangi (kulia) akikabidhi vitanda 20, magorodo 20 na mashuka 100, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13 kwa hospitali ya Wilaya ya Kisarawe mwishoni mwa wiki. Anayekabidhiwa vifaa hivyo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Bwana Hamis Likupotile (kushoto) na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt Elizabeth Oming'o. Makabidhiano hayo yaliyafanyika hospitali hapo. 

No comments

Powered by Blogger.