Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli amekabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa
hosipitali ya wilaya ya Chalinze, Ikiwa ni utekelezaji wa ilani
na ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa wananchi ikiwa
ni pamoja na wa jimbo la Chalinze.
Gari hilo la kubebea wagonjwa limekabidhiwa
kwa niaba ya Rais, na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani
Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi
gari hilo, Katibu Mkuu Ikulu Ndugu Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Mheshimiwa
Rais kwa hosipitali hiyo ikiwa ni kuitikia wito na utekelezaji wa ilani na ahadi
ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi
wake kote nchini.
Post a Comment