Waziri wa Ardhi WILLIAM LUKUVI aongoza Mazishi ya JOSEPH MUNGAI
Familia ya Marehemu Joseph Mungai ikiwa imeshikana mkono ishara ya upendo wakati wa mazishi ya baba yao. |
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika mazishi. |
Waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye akitoa salamu zake kwa niaba ya mwenyekiti wa Taifa wa Chadema. |
Heshima za mwisho... |
WAZIRI
wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi ,Wiliam Lukuvi aongoza mamia
ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa waziri wa Elimu na
mbunge wa mstaafu wa jimbo la Mufindi kaskazin Joseph Mungai
Akizungumza
katika ibada ya mazishi jana mjini Mafinga wilaya ya Mufindi ,Lukuvi
ambae alimwakilisha Rais Dkt John Magufuli alisema kuwa Mungai atakumbukwa kwa
uongozi wake uliotukuka hasa katika misingi mizuri ya elimu wa Elimu ya
Sekondari (MMES}
Lukuvi alisema kuwa
wakati serikali ilipoanzisha suala la Sekondari za Kata, Mafinga na
Mufindi kwa ujumla mwamko huo ulishaanza toka miaka ya 1980 ambayo kwa uongozi
wake kama Mbunge alihamasisha Wananchi kutoa michango, kufyatua
matofalina kina mama kuchota maji yote hiyo nji katika kufanikisha
adhima ya kusogeza elimu ya sekondari kwa watu wengi
“Alianza kuwa kiongozi akiwa na umri mdogo kuliko wanasiasa wote
wa Mkoa wa Iringa wakati huo, lakini pia alikuwa kiunganishi pale kunapotokea
misuguano yoyote hakuwa na makuu na kama ulikuwa ukitaka ushauri basi utaupata
kwa mzee wetu mungai ,” alisema.
Akiongoza ibada ya mazishi askofu wa kkkt dayosisi ya Iringa Dkt Owdenburg Mdegeka
alisema kuwa kila mwanadamu aishie chini
ya hili jua anapaswa kuishi maisha ya kumuabudu mungu na kuachana na tabia ya
kuhukumiana hapa duniani kwakuwa kila mtu atajibu dhambi zake akiwa mbingguni .
Dkt Mdegela alisema Mungai ni moja kati
ya viongozi wachache waioacha historia kubwa hapa nchini kutokana na uongozi
wake uliotukuka wa kupigania maendeleo ya watanzania bila ya ubaguzi wa Aina
yoyote
“Leo tumempoteza mtu muhimu sana
ndugu yangu Lukuvi mimi na wewe tunapaswa kukaa chini na kuangalia mustakabali
wa mkoa wetu wa Iringa ameondoka mzee Peter Siyovvela
ameondoka Adam Sapi na leo ameondoka mzee wetu Mungai sasa ni wakati
wetu kwani kwa iringa tumebaki mimi na wewe sasa tukutane kabla mwaka haujaisha
ili kujadili jambo hili alisema” Mdegella
SUMAMAYE
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia
na maendeleo Chadema Waziri Mkuu mstafu Fredrick Sumaye Alisema kuwa Taifa la
Tanzania kimepoteza kiongozi makini aliyekuwa na uthubutu wa kutenda mambo bila
ya ubaguzi na kusimamia kile anacho kiamini katika kuwatumikia watanzania
Alisema kuwa Mungai alikuwa ni mtu
mchapakazi aliyekuwa na hoja alizozijenga na kuzisimamia kikamilifu kwani
alitamani sana kutenda mambo kwa haki bila ya kubaguana kiitikadi bali
alisimama katika haki.
Alisema kuwa chama cha demokrasia na
maendeleo chadema kimesikitiswa sana na kifo chake kwani alikuwa ni mtu mpenda
demokrasia hivyo katika muuenzi na kutambua mchango wake Hapa nchini watanendeleza
kudumisha misingi mizuri ya demokrasia aliyokuwa akiishi marehemu Mungai.
Luhavi
Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu wa
chama cha mapinduzi Rajabu Luhavi
alisema Mungai atakumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka kwa wa
kuwatumikia watanzania bila ya ubaguzi
“Alikuwa kiongozi mzuri tangu uongozi wa Hayati Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Ametoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi
yetu, tunapaswa kuenzi yale mazuri waliyoyafanya na sisi tunaanzia pale
alipoishia
Akizungumza wasifu wa marehemu Denis Mungai alisema kuwa Mungai
aliwahi kuwa Mbunge wa Mufindi kupitia CCM kwa miaka 35.
Pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini enzi za
utawala wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na pia katika awamu za
pili, tatu na nne.
Baadhi ya nyadhifa alizowahi kushika kwa nyakati tofauti ni
uwaziri wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, Waziri wa Kilimo na
Maendeleo ya Mifugo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. katika utawala wake,
Mungai alifuta Umoja wa Michezo wa Shule za Msingi (UMISHUMITA) na Umo
Wabunge
Baadhi ya wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Iringa wakizungumzia
Mungai huku kila mmoja akisema alikuwa kiongozi mkweli aliyesimamia alilokuwa
analiamini.
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema),
alisema Mungai alikuwa kiongozi wa wazi asiyegopa kusimamia ukweli.
Alisema amepokea kwa mshtuko taarifa ya msiba huo
na kubainisha kuwa alimfahamu Mungai akiwa nje ya ulingo wa siasa.
“Alikuwa kiongozi mzuri tangu uongozi wa Hayati Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Ametoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi
yetu, tunapaswa kuenzi yale mazuri waliyoyafanya na sisi tunaanzia pale
alipoishia.
“Alikuwa kiongozi muwazi na alituunga mkono wapinzani ingawa
hakushinda… kwa ujumla alikuwa mtu mkweli asiyefungamana na siasa za upande
wowote,” alisema Msigwa.
mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi alisema
kuwa , watu wa Mafinga na Mufindi kwa ujumla wamempoteza mtu muhimu sana
kwani atakumbukwa kwa mengi aliyofanya hasa mwamko na kuisogeza
elimu ya sekondari kwa watu wa kawaida kupitia Mufindi Education Trust-MET,
Chumi alisema kuwa wakati serikali ilipoanzisha suala
la Sekondari za Kata, Mafinga na Mufindi kwa ujumla mwamko huo ulishaanza toka
miaka ya 1980 ambayo kwa uongozi wake kama Mbunge alihamasisha Wananchi kutoa
michango, kufyatua matofalina kina mama kuchota maji yote hiyo nji katika
kufanikisha adhima ya kusogeza elimu ya sekondari kwa watu wengi.
“Kwa jitihada mzee Mungai Mufindi ndio Wilaya ya
Kwanza hapa nchini kuwa na Bank ya Wananchi yaani Community Bank (Mucoba)
ambayo imeendelea kuwa kimbilio la tabaka la chini na Kati katika suala zima la
mikopo na huduma za kibenk mimi ,Nawaombea faraja wanafamilia wote katika
kipindi hiki cha majonzi, Mungu ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi , Amina
alisema chumi ”.
Post a Comment