Header Ads

Washiriki wa tiGO FIESTA Super Nyota Watambulishwa Jijini Dar es Salaam

 Mratibu wa Tamasha la Fiesta 2016 kutoka Tigo, Balla Shareeph(kushoto) akiongea na waandishi wa habari  kutambulisha udhamini wa Tigo kwenye shindano la Super Nyota, jumla ya washiriki 16 walipatikana mikoani ambao watashindana siku ya ijumaa kwenye fainali na kupata washindi wawili, Wengine pichani mshiriki Galla Bway(katikati) na Mratibu wa shindano la Super Nyota toka Clouds Nickson George.

Mratibu wa shindano la Super Nyota toka Clouds Nickson George(kulia)akiongea na waandishi wa habari kutambulisha washindi wa Super Nyota 16 waliopatikana mikoani ambao watashindana siku ya ijumaa kwenye fainali na kupata washindi wawili.

Mratibu wa Tamasha la Fiesta 2016 kutoka Tigo, Balla Shareeph(kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu mshiriki wa Super Nyota, Galla Bway wa Dsm kwa niaba wenzie 16, Kulia ni Nickson George kutoka Clouds Media.
.......................................

Dar es Salaam  Novemba 1, 2016 Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania  leo imewatambulisha washindi 16 wa shindano la Tigo Fiesta Super Nyota lililofanyika katika mikoa 15 ya Tanzania Bara. 

Shindano hilo lililoratibiwa na Kampuni ya Prime Time Promotions liliendeshwa katika mikoa  hiyo kwa kipindi cha miezi miwili na nusu. 

Mshindi wa fainali yake atajulikana wakati wa fainali ya mwisho Novemba 5, 2016 itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari  wakati wa kutangaza washindi hao, Mratibu wa mradi wa Tamasha la Fiesta 2016 kutoka Tigo, Balla Shareeph alisema, “ Tigo inaona fahari kuinyanyua sekta ya muziki ya Tanzania  kwa kuwapatia  wasanii  wanaoibukia  jukwaa la kuonesha  vipaji vyao waweze kufikia kiwango cha juu nchini na  wakati huo huo kuwawezesha kutambuliwa na chapa mbalimbali za muziki.”

Shareeph aliwapongeza  washindi  kwa kutumia nafasi hiyo kuwakumbusha  wao wenyewe pamoja na umma kwa ujumla kwamba wanaweza kupata tiketi  zao kwa  ajili ya fainali hiyo ya kuhitimisha tamasha la Fiesta 2016 ambalo litafanyika  katika viwanja vya Leaders Novemba 5, 2016  kwa kutumia mtandao wa Tigo Pesa.

Shareeph alifafanua, “Ili kupata tiketi kupitia Tigo Pesa  wateja wote wa Tigo na wasio katika mtandao huu  wanatakiwa kulipia tiketi kwenda namba 0678 888 888. Mkakati huu unalenga kuwapatia Watanzania njia ya kawaida na rahisi  ya kupata tiketi zao.”  

Washindi  Super Nyota 16  ambao majina yao ni Nchama Anton a.k.a Nchama, Raphael  Charles  Manengo  a.k.a Manengo kutoka (Mwanza), Ibrahim Juma   a.k.a   Mpanduji(Shinyanga) , Obed  Moses   a.k.a    O strings(Muleba), Salum Asman   a.k.a  Alinacha ( Kahama), Gasper Festo    a.k.a   YOW (Tabora)  Alex Joseph    .a.k.a  TIZO( Singida), Godfrey Andrew Mhoja  a.k.a  NEXUS( Dodoma) Hamad Hussein  a.k.a  Med Botion (Morogoro)  Cyril Henry Isidor a.k.a So Real(Tanga) Wilson Pascal     a.k.a  Willy Desmiller( Mtwara )   Charles Mariki  a.k.a Gerere(Moshi)    Mohammedy  Amiry  a.k.a  Croozy (Arusha), Amina Chibaba    a.k.a  Ammy Chiba  (Mbeya)   Leonard John  Haule   a.k.a sauti classic (Sumbawanga)    wata zawadiwa simu ya kisasa ya Tecno  Y3+ Music, ikiwa na muda wa maongezi.

 Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Mratibu wa shindano la Super Nyota  chini ya mrengo wa Tamasha la Fiesta 2016, Nickson George ambaye alisema, “Tunayofuhara  kubwa kutangaza  kwamba washindi 16 Super Nyota  ambao watashiriki katika Fainali Kuu  ya Fiesta 2016. 

Tunatarajia  kuendelea kishukuru jamii kwa kuandaa shindano kama hili  katika kuinyanyua sekta ya muziki na burudani ndani ya Tanzania.”

Tamasha ya Tigo Fiesta 2016  ni tukio linaloendeshwa kwa ubia baina Kampuni ya Prime Time Promotions na Tigo Tanzania na wakati huo huo Tigo ikiwa ndio mdhamini mkuu.

No comments

Powered by Blogger.