( VIDEO ) Serikali yakana Shutuma za Kumtelekeza Mshindi wa Miss Tanzania 2016
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amesema serikali haijamtelekeza mshindi wa shindano la Urembo la Tanzania kwa mwaka 2016 bali wanaendelea kumpa msaada wa hali na mali ili kufanikisha ushiriki wake katika mashindano ya urembo ya dunia.
Mhe. Nape ameyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi Bendera ya Taifa kwa mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano ya Miss Afrika 2016 yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu.
“Haiwezekani Serikali ikabariki mchakato mzima wa Miss Tanzania mshindi akapatikana alafu akatelekezwa na tukakaa kimya sio kweli” Alisistiza Mhe. Nnauye.
Mhe. Nnauye ameongeza kuwa watanzania wawe na desturi ya kutangaza mambo mema yanayotokana na shindano hilo la urembo badala ya kutafuta mapungufu na kuyakuza na yakaonekana kuwa ni tatizo kubwa katika machakato huo.
Aidha amewahakikishia watanzania kuwa Miss Tanzania yuko salama na atashiriki vizuri katika mashindano ya Miss World kwa mwaka 2016 watanzania wazidi kumwombea na ikiwezekana kwa mwaka huu mrembo wa Dunia atokee Tanzania.
Katika mashindano ya urembo kwa mwaka 2016 mrembo yaliyofanyika Jijini Mwanza na Bi Diana Edward Luqumay alishinda taji hilo na anatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia 2016 yatakayofanyika mwishoni mwa mwaka huu Washington Dc nchini marekani na yatashirikisha nchi 119.
Post a Comment