Wanafunzi wa kidato cha nne wakimsikiliza naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi selemani jafo mara baada ya kukagua maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika Leo.
...............
Naibu
waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani
Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma kuangalia maandalizi
kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo nchini.
Katika ziara yake kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha
ndege na Msalato, Jafo amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na
vitendo vya udanganyifu.
Akizungumza na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo
amesema katika mtihani huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa
wamejifunza kupitia mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya
walimu kujificha chooni ili kuwasaidia wanafunzi.
Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake.
Ameeleza hatarajii mitihani hiyo ifanyike kinyume na kuwataka
walimu wasisubutu kufanya udanganyifu wowote na kuziingiza shule zao kwenye
kashfa.
Jafo ame sema mara nyingi mitihani hiyo inapofanyika kumekuwa na
wizi wa mitihani na kutofuatwa kwa taratibu za mitihani.
Akizungumza na wanafunzi, Jafo amewataka kujiepusha na vitendo
hivyo kwa kuwa vitawafanya wafutiwe mitihani na kupoteza malengo yao kwenye
maisha.
Hata hivyo amewahakikishia walimu kuwa serikali ya awamu ya tano
imejipanga kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na kuwataka
kuwajibika ipasavyo.
|
Post a Comment