Rais
wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa
akizungumza katika hafla fupi ya kumkabidhi tuzo na kumvisha nishani Dkt.
Fredrick Kigadye aliyotunukiwa na Baba Mtakatifu Papa. Francis mapema wikiendi hii, Kushoto ni Mhadhama
Kardina Polycarp Pengo, Dkt Fredrick Kigadye na Mkewe.
.............................
Jamii imeaswa kufanya
kazi kwa uadilifu, uaminifu, weledi na uzalendo wa hali ya juu ili wapate
kuheshimika na kuthaminiwa na jamii zinazowazunguka kwa kutambua mchango wao
katika kuendeleza jamii.
Hayo yamesemwa na
Mhadhama Kardinali Polycup Pengo wakati wa hafla ya kumkabidhi nishani ya Benemerenti (Anayestahili), Dkt. Fredrick Kigadye, ambayo
utolewa na Baba Mtakatifu kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kulitumikia Kanisa
na jamii kwa ujumla jana Jijini Dar es Salaam.
“Ni vyema tukatambua
ya kwamba kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio
mahali pepote pa kazi na katika maisha yetu ya kila siku”. Alisema Kardinali
Pengo.
Kwa upande wake Rais
wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa masema
kuwa Dkt. Kigadye amekuwa mtumishi wa wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa
muda wa miaka 35 huku akifanya kazi katika Idara ya Afya katika Hospitali ya Rufaa
ya Bugando kwa mafanikio makubwa.
Ameonesha ni namna
gani watu tunapaswa kujitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu kupitia vipawa na
taaluma tulizo jaaliwakuwa nazo hii inatia moyo sana. Aliongeza Askofu
Ngalekumtwa.
Akizungumzia Tuzo
hiyo aliyopewa na Baba Mtakatifu Papa Francis, Dkt Kagadye amesema kuwa
anajisikia mwenye furaha kubwa na wathamani kwa kupewa tuzo ya heshima na
kiongozi mkubwa duniani nakuongeza kuwa tuzo hiyo inamuongezea chachu ya kuishi
katika misingi imara ya maadili na weledi.
|
Post a Comment