WAZIRI MATHIAS CHIKAWE, ATANGAZA MAFANIKIO YA WIZARA YAKE, KATIKA KIPINDI CHA MIAKA KUMI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne.
Chikawe alisema
kupitia taasisi zake yakiwemo Majeshi ya Polisi, Magereza, Uhamiaji,
Zimamoto na Uokoaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Idara ya
Wakimbizi pamoja na Idara zingine zilizoko chini ya wizara hiyo, imepata
mafanikio makubwa hususani katika jukumu la msingi la ulinzi na usalama
wa nchi jambo ambalo limewezesha nchi kuwa na amani na utulivu. Kikao
hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar
es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya
wizara yake katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne.
Chikawe alisema
kupitia taasisi zake yakiwemo Majeshi ya Polisi, Magereza, Uhamiaji,
Zimamoto na Uokoaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Idara ya
Wakimbizi pamoja na Idara zingine zilizoko chini ya wizara hiyo, imepata
mafanikio makubwa hususani katika jukumu la msingi la ulinzi na usalama
wa nchi jambo ambalo limewezesha nchi kuwa na amani na utulivu.
Kikao
hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar
es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini (D-IGP), Abdulharman Kaniki akijibu swali la mwandishi wa habari
kuhusu uwepo wa vituo vidogo vya polisi nchini (Police Posts) pamoja na
majukumu yake.
Kwa mujibu wa D-IGP, vituo hivyo vipo kwa mujibu wa
sheria na haviruhusiwi kuwa na silaha za moto, na endapo askari wa vituo
hivyo vidogo wakimkamata mtuhumiwa watampeleka katika vituo vikubwa vya
polisi ili utaratibu mwingine wa kisheria uweze kufanyika.
Kiongozi
huyo wa Polisi alipewa nafasi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe ili kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu vituo hivyo, wakati wa
mkutano na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya wizara katika
Serikali ya Awamu ya Nne, uliofanyika katika Ukumbi wa wizara hiyo,
jijini Dar es Salaam leo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa
ya Jinai (DCI), Diwani Athuman.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Post a Comment