Header Ads

TAKWIMU: Watanzania Bado Wanakabiliwa na Tatizo la Udumavu wa Akili na Mwili

Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Mkutano wa uhamasishaji wa Afya na lishe kwa vijana (hasa kwa wasichana),Mkurugenzi wa Kinga,Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt.Neema Rusibamayila akisoma hotuba wakati wa mkutano huo ambao wa siku tatu unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt.Joyce Kaganda akizungumza kwenye mkutano huo.

Baadhi wa washiriki wa mkutano huo wakifuatilia uwasilishaji wa mada.Mkutano huo wa Kimataifa unawashirikisha viongozi wa juu wa serikali, mashirika na taasisi binafsi pamoja na wadau wa maendeleo nchini na nje ya nchi.

....................................



Takwimu ya hali ya lishe nchini kwa mwaka 2015/16
inaonyesha kuwa bado kuna uwepo wa hali ya tatizo
la udumavu kwa watanzania hususani katika udumavu
wa akili na mwili.

Akizungumza hayo Dar es Salaam jana,Mkurugenzi
Msaidizi wa Lishe wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,Dkt Vicent Assey
wakati wa mkutano wa wadau mbalimbali wa
Afyanchini, alisema sababu kubwa inayosababisha
watoto kuzaliwa na hali ya udumavu ni kutokuwepo na
mpangilio mzuri wa vyakula.

Alisema jamii bado inachangamoto ya kutojua lishe
bora kwa wakati muafaka inayozingatia mlo kamili na
kujua ni wakati gani chakula kinatakiwa kuliwa kwa
mtoto.

Dkt Assey alisema serikali inaendelea kuweka nguvu
katika kusaidia kutatua tatizo hilo ambapo hadi
sasa tatizo hilo limepungua kutoka asilimia 42 hadi
34.

Alisema kutokana na takwimu hizo inaonyesha hali
imeanza kuwa nzuri kwa kutatua  tatizo hilo ambapo
kuna baadhi ya mikoa iliyofanya vizuri katika
kutokomeza hali hiyo ikiwemo Dar es Salaam
ikionmyesha hali ya udumavu ni asilimia 14.6 huku
mikoa mingine bado hali yake sio nzuri katika
tatizo hilo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkazi wa taasisi ya
Micro  nutrient inifiative,Dkt Daniel Nyagawa
alisema mkutano huo umejumuisha wadau mbalimbali
kutoka serikalini,mashirika ya kimataifa,taasisi
zisizokuwa za kiserikali kutoka katika nchi nne
ikiwemo Senegal,Ethiopia,Kenya na Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.