Header Ads

Komredi KINANA aongoza Mazishi ya EDWIN MSELLE mkoani Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu mkoa wa Kilimanjarona Mjumbe wa Mkutano  Mkuu wa CCM, Edwin Mselle, wakati wa ibada na kuaga mwili, wakati wa mazishi, yaliyofanyika leo Wilayani Kibosho, mkoani Kilimanjaro. 

Edwin ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa udaktari, mwaka wa nne katika Chuo Kikuu Kishiriki cha KCMC, ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM waliofariki kwa ajali ya gari, wakati waitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, Februari 5, 2017 ambapo Kinana ameongoza kwenye mazishi yao wote.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu mkoa wa Kilimanjarona Mjumbe wa Mkutano  Mkuu wa CCM, Edwin Mselle, wakati wa ibada na kuaga mwili, wakati wa mazishi, yaliyofanyika leo.
Marehemu Edwin Mselle enzi za uhai wake.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Mecky Sadick kwenye mazishi hayo.
Waombolezaji.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaliiana na Paroko wa Kanisa Katoliki Mwika, Emmanuel tumaini wakati wa mazishi hayo.
Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi na waombolezaji wengie kwenye mazishi hayo.
Upande wa wa Ndugu wa Marehemu wakiwa kwenye mazishi hayo.

Ibada ya kuombea marehemu ikifanyika wakati wa mazishi hayo.


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi zake binafsi, CCM na za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli wakati wa mazishi hayo.

Kinana akikabidhi rambirambi kutoka CCM na Jumuia zake kwa Baba wa Marehemu Edwin, Christopher Mselle wakati wa mazishi hayo.

Vijana wa UVCCM wakiwa wamebeba jeneza kwenda eneo la maziko, wakati wa mazishi hayo.

Huyu kuku naye alihudhuria mazihi hayo, na wengi kutafsiri kwamba, Marehemu amezikwa kwa baraka sana.
Taratibu zikifanywa na Padre kabla ya kuingiza jeneza kaburini.

Padre akisoma maandiko matakatifu ya biblia kabla ya mwili kuingizwa kaburini.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa kaburini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka udongo kaburini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akimwaga udongo kaburini wakati wa maziko.
Baba na Mama wa marehemu wakiweka udogo kaburini. 

No comments

Powered by Blogger.