Mbunge MZUZURI awahimiza Vijana Kutumia fursa za Kilimo ili Kujikwamua Kiuchumi
Mbunge wa Viti maalum kundi la vijana Mariam Ditopile Mzururi akiwa na vijana wa CCM wakielekea kwenye shamba la Zabibu la Chinangali lililopo Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Mbunge wa viti maalum
kundi la vijana Mariam Ditopile Mzuzuri akiwa na vijana wa CCM katika shamba la
zabibu lililopo Chinangali wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Wabunge wa viti maalum
Mariam Ditopile Mzuzuri na Maria Kangoye wakiwa na vijana wa CCM akiwemo msanii
Jokate Mwegelo wakipewa elimu ya namna ya kuotesha zabibu, changamoto zake na
faida ya zao hilo.
Mbunge wa Viti maalum kundi la vijana Mariam Ditopile Mzuzuri akizungumza na vijana wa CCM
aliombatana nao kutembelea mashamba ya zabibu wilayani Chamwino mkoani Dodoma akieleza dhamira ya kuwapeleka katika shamba hilo.
.........................................................
MBUNGE wa viti maalum Mariam Ditopile Mzuzuri amewasihi vijana
kujishughulisha na shughuli za kilimo hususan kilimo cha zabibu ili kujiinua
kiuchumi na kuondokana na tatizo la ajira.
Hatua hiyo ni kuunga mkono na kutekeleza kwa vitendo kauli
mbiu ya Rais Dk.John Magufuli ya hapa kazi tu na kuwa na Tanzania ya
Viwanda.
Mariam alitoa rai hiyo mjini hapa wakati alipofanya ziara
ya kutembelea Shamba la Zabibu la Chinangali II, akiambatana na vijana wa
Chama cha Mapinduzi kwa lengo la kujifunza namna ya uzalishaji, ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM.
Alisema imefika wakati warudi na kuitekeleza kauli ya kama
unataka mali utaipata shambani, ambayo itafanikiwa kwa watanzania kuwekeza
kwenye shughuli za kilimo.
" kimsingi Zabibu ya Dodoma licha ya kutumika kutengeneza
mvinyo ambao unasafirishwa ndani na nje ya nchi lakini bado haijatangazwa kiasi
cha kutosha na kusababisha soko lake kuwa chini,"alisema Mariam.
Alisema imefika wakati vijana wa CCM kutumia fursa hiyo ikiwa ni
pamoja na kuitangaza Zabibu ya Dodoma, na hasa ukizingatia kipindi hiki ambacho
nchi inakwenda kuwekeza katika viwanda.
“Mimi kijana mwenzenu nawasihi mtumie vyema fursa hii ili muweze
kujikwamua kiichumi, nimetumia nafasi hii kuwaleta ili mje kujifunza namna
kilimo cha Zabibu kinavyotekelezwa ili nanyi muweze kuiga mfano huo kwa
vitendo,”alisema.
Naye Mbunge wa Viti Maalum, Maria Kangoye aliyeambatana na
Mariam katika ziara hiyo, aliisihi serikali yake sikivu ya CCM
kuhakikisha inawawezesha vijana kikamilifu kupitia ile asilimia 5, ambayo ipo
kisheria na imekuwa ikitengwa wakati wote.
Pia aliwasihi vijana wa CCM, kuacha kubweteka na badala yake
wafanye kazi na kujitokeza kushiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo.
Kwa upande wake Jokate Mwogelo ambaye pia aliambatana na mbunge Mariam katika
ziara hiyo aliwataka vijana kutotumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii
kwa kuzungumza mambo yasiyofaa.
"Sisi vijana wa CCM tubadilike, tutumie mitandao hii
kujiinua kiuchumi, tuelezane na kupashana habari za fursa zilizopo na hapo
tutafanikiwa, alisema Jokate.
Shamba hilo la Zabibu la Chinangali II, hadi kufikia Julai 2016
lilikuwa na jumla ya ekari 295 ambazo zimeendelezwa kwa ruzuku kutoka serikali
kuu na halmashauri ya wilaya ya Chamwino na mkopo wa Benki ya CRDB wa jumla ya
Sh.bilioni 1.5.
Pia shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 1,250 lilianzishwa
mwaka 2008 na likikusudiwa kutoa mchango mkubwa wa kupunguza umasikini
kwa vijana, wanawake na kutoa ajira kwa jamii ya vijiji sita vinavyozunguka
eneo la mradi.
Post a Comment