Header Ads

Mkuu wa mkoa wa Iringa AMINA MASENZA aonya Watumishi Wanaokwepa Mazoezi ya Viungo


Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  mwalimu  Amina Masenza (wa tatu kushoto) akiongoza  mazoezi ya viungo katika  uwanja wa  samora  Leo wa  pili kushoto ni katibu  tawala wa mkoa  wa Iringa wamoja Ayubu.

............................................

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa mwalimu  Amina Masenza amewaonya  watumishi  wa serikali ambao wanakwepa  kushiriki mazoezi ya  pamoja katika  uwanja  wa  Samora  na  kuwa kuanzia sasa mtumishi atakayekwepa kushiriki  kubanwa .

Alisema pamoja na kuwa mazoezi  hayo ni kwa ajili ya afya za kila mmoja kujikinga na maradhi  yanayosababishwa na  kutofanya mazoezi ila  bado mazoezi hiyo  ni  utekelezaji wa agizo la makamu  wa Rais kwa  kila mtanzania .

Hivyo  alisema kutokana na baadhi ya  watumishi hasa  wanawake  kukwepa mazoezi hayo anaandaa mkakati wa kuwabana  watumishi  wote  wanaokwepa mazoezi kwa  kuitisha mazoezi  siku ya kazi ili wale  ambao  watashindwa  kufika watawajibishwa .

"Naangalia  ni  siku gani  ambayo  itakuwa ni  siku ya kazi kama ijumaa ama siku  nyingine  yeyote  ambayo  nitaitisha mazoezi kuanzia ofisi  yangu  hadi  Samora kwa  kila mtumishi kushiriki na siku hiyo hata ofisini  watumishi  wakichelewa ni  sawa lengo  kuweza  kufanya mazoezi na kutekeleza agizo la  serikali ......nashangazwa  sana  awali  wanawake  ndio  ambao  walikuwa  wakifika kwa  wingi mazoezini  ila leo  hii idadi ya  wanawake  imepungua ukilinganisha na  wanaume ....nawashangaa sana wanawake  wanaokwepa mazoezi  wakati  ndio ambao  wanakula vitu  vyenye mafuta "

Hivyo  alisema  kuanza sasa  kila mtumishi  wa serikali  lazima  kufika katika mazoezi na  utawekwa  utaratibu  wa  kuorodhesha majina kila idara  ya  watu  wanaoshiriki mazoezi .

DC  Iringa  Richard  Kasesela wa kwanza  kulia  akishiriki mazoezi ya  riadha kutoka  uwanja  wa Samora.

Washiriki wa  mazoezi  wakiwasili  ufisi ya  RC Iringa wakitokea  uwanja  wa  Samora.


Afisa  michezo mkoa wa Iringa Kenedy Komba  akiorodhesha  majina  ya wakuu wa Idara  walioshiriki mazoezi leo ni  kuwabana wamnaokwepa mazoezi.


Wanamazoezi  wakitoka  uwanja wa  samora.



No comments

Powered by Blogger.