Header Ads

BURIANI: Jennifer Livigha ( CHINGA ONE ) Wengi wajitokeza Kuuaga Mwili wake

Pichani Mpendwa wetu Jennifer Livigha aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la Chinga One na Mwanachama wa TBN Enzi za uhai wake. 

Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. 

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. 

Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.

 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Jennifer Livigha aliyekuwa mmiliki wa Blog ya Chinga One katika Hospitali ya Amana.

 Waongozaji wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jennifer.

 Waombolezaji wakiwemo baadhi ya wana Tanzania Bloggers Network (TBN) ambapo Marehemu Jennifer alikuwa mwanachama.

 Mmoja ya waombolezaji akitoa historia fupi ya Marehemu.

Mmoja wa wanafamilia akitoa utaratibu kabla ya kuanza kutoa heshima za Mwisho kwa mpendwa wetu Jennifer

 Baadhi ya wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN) wakiwa wanaaga mwili wa aliyekuwa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer 'Chinga One'.

Baadhi ya wanachama wa TBN , ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wanapeleka mwili wa Marehemu Jennifer katika Gari tayari kwa safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi.

Baadhi ya wanafunzi wakilia kwa uchungu.
Picha zote  na Fredy Njeje 

No comments

Powered by Blogger.