Header Ads

Mkuu wa Wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA afanya ziara ya Ukaguzi wa Vipimo na Mizani Feki

Mkuu wa wilaya ya Ilala, kwa kushirikiana na Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), mkoa wa Ilala, amefanya ziara ya kustukiza katika maeneo mbalimbali, katika kampeni yake ya kudhibiti vipimo na mizani 'feki'. Pichani, Mjema akikagua mzani kwenye bucha moja eneo la Kariakoo, Dar es Salaam, akiwa katika ziara hiyo, Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na kulia ni mfanyakazi katika bucha hiyo, Omar Khalfan.


MWANZO WA ZIARA HIYO
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia) na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Edward Mpogolo (kushoto) wakiwa katika Ofisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), mkoa huo wa Ilala, baada ya kuwasili kwa ajii ya kuanza ziara ya kustukiza kukagua vipimo na mizani feki, katika maeneo mbalimbali leo. Aliyesimamani mwenyeji wao, Kaimu Meneje wa WMA mkoa huo wa Ilala, Alban Kihulla.
Kaimu Meneja wa WMA mkoa wa Ilala, Alban Kihulla, akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia), jinsi ya kutofauisha mizani 'feki' na ile iliyo bora, kabla ya kuendelea na ziara nje ya ofisi hiyo. 
Mjema akionyeshwamizani malimbali feki na iliyo bora, katika karakana ya WMA mkoa wa Ilala.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na wapokea mizigo hasa ya viazi mviringo, katika mitaa ya Kariakoo, Dar es Salaam, kuhusu umuhimu wa akuepuka kupokea magunia yaliyojazwa kwa mtindo wa Lumbesa, kwa kuwa utaratibu huo unakiuka vipimo halisi na hivyo kutia serikali hasara kwa kuwa siyo kipimo halali.
Mjema akiwa fafanulia zaidi kuhusu hasara ya Lumbesa.

Mjema akizungumza na wananchi na waandishi wa habari baada ya kumaliza sehemu ya ukaguzi wake wa vipimo na mizani, Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo. 

(Picha zote na Bashir Nkoromo).

No comments

Powered by Blogger.