Header Ads

Katibu Mkuu wa CCM, Komredi KINANA aongoza Mazishi ya Mjumbe wa NEC

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wa sita kulia) akishiriki kuswalia  jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa NEC, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Mwalimu Ali Mbaga, wakati wa mazishi yaliyofanyika leo Feb 8, 2017, katika kijiji cha Kighare, Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Mbaga ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM, waliofariki kwa ajali ya gari wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM katika mkoa huo.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro, leo tayari kwenda kuongoza mazishi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Ally Mussa Mbaga, katika kijiji cha Kighare, Wilayani Mwanga katika mkoa huo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha wagenikatika Ofisi hiyo. Wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Iddi Juma na kulia ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Deogratius Ruta.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiongoza kwenda  nyumbani kwa marehemu Mbaga, kuongozamazishi hayo.

Naibu Katibu Mkuu wa CWT, Oluochi akitoa salama za rambi rambi kwenye mazishi hayo.

Waombolezaji wakitoa ndani jeneza lenye mwili wa marehemu Mbaga kwa ajili ya kuswaliwa na kuzikwa mwili huo wa marehemu.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Watatu kulia walioko mstari wa mbele, akishiriki kuomba dua wakati wa kuswalia mwili wa marehemu Mbaga, wakati wa mazishi hayo.

waombolezaji wakifikisha eneo la kaburi jeneza lenye mwili wa marehemu mbaya tayari kwa maziko.

Mwili wa marehemu Mbaga ukishushwa kaburini.

Waombolezaji wakizika.

 PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments

Powered by Blogger.