Header Ads

Waziri SIMBACHAWENE ateta na Viongozi wa CWT Kuhusu Madai ya Walimu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)  George Simbachawene  akisikiliza maelezo ya madai ya Walimu  kutoka kwa Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Ezekiel Oluoch katika mkutano ulofanyika katika ofisi za TAMISEMI kujadiliana juu ya madai ya Walimu leo mjini Dodoma. 

Mkutano huo ulihusisha ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Tume ya utumishi ya Walimu (TSC), Wizara ya Fedha na Mipango, na Ofisi ya Rais Utumishi. 

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI)   George  Simbachawene  akiongea na wajumbe wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) katika mkutano uliofanyika katika ofisi za TAMISEMI kujadiliana juu ya madai ya Walimu leo  Dodoma. 

.................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amekutana na viongozi wa chama cha Walimu nchini (CWT) na kuzungumza nao baada ya kutangaza mgogoro na serikali ifikapo Machi Mosi, mwaka huu, iwapo madeni ya walimu hayatashughulikiwa.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Tamisemi mjini Dodoma ambapo Waziri Simbachawene aliwashukuru viongozi wa CWT pamoja na ofisi ya utumishi kwa kuweza kukaa pamoja ili kuepusha mgogoro huo.

Simbachawene alisema katika kikao hicho waliweza kujadiliana na walimu kuhusu madai yao kutokana na taasisi hiyo kuwapo chini ya Tamisemi, hivyo lazima wakae pamoja.

Alisema anashukuru hatua ya viongozi wa CWT wakiongozwa na Rais Gratian Mkoba na Katibu Mkuu Ezekiel Oluoch, kwa kukubali kukaa pamoja na serikali kuhusu kunusuru mgogoro wanaotarajiwa kuutangaza na kwamba serikali imeyapokea yote na kupata muda wa kuyajadili.

Alisema kwa kawaida mahali popote, lazima kuwepo na madai ya mwajiri na mwajiriwa, hivyo serikai imeyapokea madai ya walimu hao na kuyapitia kisha kuyatolea maamuzi.

No comments

Powered by Blogger.