Header Ads

Watanzania Washauriwa Kutumia Fursa ya Kuwekeza Mkoani SIMIYU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akisisitiza jambo wakati akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu.
......................

Na Mathias Canal, Simiyu

Wafanyabiashara na wadau wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kutumia fursa za uwekezaji wa biashara hususani katika kuwekeza kwenye viwanda kwani mipango mingi inayopangwa na serikali inatoa fursa zaidi kwa wawekezaji wa ndani ya nchi jambo ambalo litaifanya Tanzania kuondokana na umasikini kutokana na fursa zilizopo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka wakati akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu lililofanyika katika Ukumbi wa Parokia ya Mtakatifu John lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.

Rc Mtaka amesema kuwa Katika kuchochea na kuleta maendeleo  kwa wananchi katika Mkoa wa Simiyu uongozi wa Mkoa huo una dhamira ya dhati kuwafanya wananchi wake kuingia katika ramani ya Mkoa unaotumainiwa nchini.


Wadau wengine walioshiriki katika Jukwaa hilo la Biashara ni pamoja na TIB Development Bank, National Microfinance Bank (NMB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na TIB Development Bank Ltd.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel (kushoto), na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper Dkt Jim Yonazi (kulia) wakisikiliza maelezo mbalimbali katika Kongamano hilo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel akisisitiza umuhimu wa Viwanda nchini Tanzanai.


Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate Bank Ltd Bi Theresia Soka (kulia) akiwa na Zacharia Kicharo Meneja wa TIB Development Bank Ltd Lake Zone wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndg Jumanne Sagin akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kuzungumza na wafanyabiashara na wawekezaji waliojitokeza katika kongamano la uwekezaji.

Kutoka Kulia ni Emmanuely Gungu Silanga Mwenyekiti wa Viwanda Mkoa wa Simiyu, Peter Bahini Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza Kusini (SNC) na Emmanuely Lupembe Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza Kusini (SNC wakifatilia kwa makini kongamano la uwekezaji Mkoani Simiyu.


No comments

Powered by Blogger.