Header Ads

Profesa MBARAWA: Ukarabati Uwanja wa Ndege wa Mtwara Kuanza Julai mwaka Huu

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akipata taarifa ya maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoani humo, Bi. Zitta Majinge (kulia), mara baada ya kuwasili leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda.
..............................

Serikali imesema  ina mpango wa kukarabati uwanja wa ndege wa  Mtwara  ifikapo mwezi Julai mwaka huu ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kutua uwanjani hapo na hivyo kufungua fursa za kiuchumi mkoani humo.

Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa ukarabati huo utahusisha njia ya kuruka na kutua ndege, maeneo ya maegesho pamoja na barabara yenye urefu wa km 1.5 inayoingia katika uwanja huo.

"Tunategemea mwisho wa mwezi huu kutangaza zabuni ya ukarabati wa uwanja huu, matumaini yetu tutampata mkandarasi mzuri kwa ajili ya kazi hii", amesema Waziri Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa amefafanua kuwa Serikali itahakikisha kuwa  inajenga uzio katika uwanja huo ili kuhakikisha usalama wa uhakika uwanjani hapo.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoa wa Mtwara, Bi. Zitta Majinge (wa pili kulia), kuhusu ukarabati wa uwanja huo mara baada ya kuwasili leo mkoani hapo. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda.

Muonekano wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambalo lina uwezo wa kubeba abiria 100 kwa wakati mmoja. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akifafanua jambo kwa Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) mkoa wa Mtwara Emmanuel Wanje, wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa Mtwara leo.

No comments

Powered by Blogger.