Zaidi ya Dola Milioni 36 Kufikisha Huduma za Mawasiliano Vijijini
Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert
Richard akimuonyesha ramani inayoonyesha maeneo ambayo mfuko umetekeleza
miradi ya kupeleka huduma za mawasiliano baadhi ya wa wananchi
waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO leo
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert
Richard akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea
banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO.
Mwanasheria wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Ambokile Mwakaje (Kulia) akimuelekeza baadhi ya maeneo walipotekeleza miradi ya huduma za mawasiliano mmoja wa mwananchi aliyetembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO.
Afisa
Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Edwin Makala
akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea banda la
mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO.
Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert
Richard akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea
banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO.
Baadhi
ya wananchi wakiwa katika banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
(UCSAF) wakati wa maonyesho ya SIMU EXPO 2016 leo jijini Dar es Salaam.
Zaidi
ya dola za kimarekani milioni 36 zimetumika katika kufikisha huduma za
mawasiliano ya simu katika maeneo ya vijijini yasiyo na mvuto wa
kibiashara nchini.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa
Wote (UCSAF) Albert Richard wakati wa maonyesho ya SIMU EXPO 2016 leo
jijini Dar es Salaam.
Mfuko
wa Mawasiliano kwa wote unashiriki maonyesho hayo ili kutoa elimu kwa
umma juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
Albert
amesema kuwa kazi kubwa ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ni kufikisha
huduma za mawasiliano ya simu katika maeneo yote ya vijini yasiyo na
mvuto wa kibiashara ambapo makampuni ya simu yanasuasua kupeleka huduma
hiyo.
“Sisi
kama Taasisi ya Serikali kazi yetu kubwa ni kufikisha huduma za
mawasiliano katika maeneo yote ya vijini ambayo makampuni binafsi
yanasuasua kupeleka huduma kutokana na msukumo wa kibiashara.” Alisema
Albert.
Aliongeza
kuwa mradi wa kwanza uliotekelezwa na mfuko huo umegharimu takribani
Dola za Kimarekani milioni 5.8 ambapo jumla ya Kata 52 zimenufaika na
mradi huu kwa kuunganishwa na huduma za mawasiliano ya simu.
Pamoja
na jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma
za mawasiliano ya simu kumekuwa na changamoto katika kutekeleza azma
hiyo kwa wakati kutokana na ufinyi wa bajeti na kukosekana kwa
miundombinu rafiki kama vile Barabara na Umeme.
Kutokana
na changamaoto hizo Albert ametoa rai kwa jamii kuwa na subira wakati
utekelezaji wa miradi ya kupeleka huduma za mawasiliano ya simu katika
maeneo yao ukiendela hatua kwa hatua kadri fedha zinavyopatikana.
Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa
mwaka 2006 kwa lengo la kupeleka na kufanikisha mmawasiliano kwa
wananchi waishio katika maeneo machache ya mijini na maeneo mengi ya
vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma ya mawasiliano.
Post a Comment