CHADEMA yakimbiwa GOODLUCK OLE MEDEYE atimkia UDP
Mwenyekiti
wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimkabidhi kadi ya uanachama
Goodluck Ole Medeye aliyekuwa mwanachama wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA leo kwenye Makao Makuu ya Chama hicho Mwananyamala
Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimshuhudia Bw. Goodluck Ole
Medeye wakati akionyesha kadi ya uanachama aliyokabidhiwa baada ya
kujiunga na Chama cha UDP akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA leo kwenye Makao Makuu ya Chama hicho Mwananyamala Kinondoni
jijini Dar es salaam.
wenyekiti wa Chama cha UDP Mzee
John Momose Cheyo akimpongeza mke wa Goodluck Joseph Ole Medeye mara
baada ya mume wake kujiunga na Chama cha UDP leo.
……………………………………
Kada wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA, aliyedumu na chama hicho kwa miezi kumi na moja
Goodluck Ole Medeye, amekihama chama hicho na kujiunga na United
Democratic Party UDP.
Bw. Medeye aliyewahi kuwa Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi
CCM na kuitumikia serikali katika nafasi ya Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ametangaza uamuzi wa kuhama Chadema
jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa kadi ya UDP na Mwenyekiti wa Chama
hicho John Momose Cheyo.
Mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Arumeru Magharibi amejiunga
na UDP akiwa na Mkewe, pamoja na watu wengine tisa wakiwemo waliokuwa
kwenye vyama tofauti na wengine waliodai hawakuwahi kuwa kwenye siasa,
ambapo katika maelezo yake, Ole Medeye amesema awali alitaka kuunda
chama kipya lakini baada ya kupitia katiba za vyama akaona UDP ni sehemu
sahihi.
Kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, wanasiasa hao
wamelaani uminywaji wa demokrasia katika kipindi hiki, hususan ndani ya
Bunge, na kushauri wabunge wa kambi ya upinzani wanaosusia vikao
kurejea ndani ya ukumbi wa Bunge kwa vile njia wanayotumia haitabadili
utaratibu wa kibunge hususan kumuondoa Naibu Spika kwenye kiti chake.
Post a Comment