TANROADS yatoa tathmnini ya Utekelezaji wa Miradi ya Barabara
Frank
Mvungi-Maelezo
Serikali
yatumia Bilioni 2 kulipa Fidia ili kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi wa
Barabara kwa kiwango cha lami kati ya Tanki Bovu na Goba Jijini Dar es salaam.
Kauli hiyo
imetolewa na Mhandisi wa Miradi wa TANROADS
Mkoa wa Dar es salaam Bw. Ngusa Julius wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es salaam.
Akifafanua
Mhandisi Ngusa amesema kuwa fidia kwa wakazi hao itakamilika kulipwa wiki hii
ili kazi ya ujenzi wa Barabara hiyo iweze kukamilishwa kwa wakati hali itakayosaidia kupunguza
msongamano wa magari.
“Ujenzi wa
barabara hii ukikamilika utasaidia kwa Kiasi kikubwa kupunguza foleni kwa kuwa
itakuwa kiungo kati ya wakazi wa Mbezi Beach na Kimara na maeneo mengine ya
jiji la Dar es salaam.” Alisisitiza Mhandisi Ngusa.
Kwa upande
wa Barabara ya kinyerezi Kifuru Mhandisi
Ngusa amesema kuwa Milioni 431 zimetumika kulipa fidia na ujenzi wa Barabara
hiyo unaendelea.
Miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lamai
inayotarajiwa kukamilika katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha 2015/2016 itasaidia kupunguza msongamano wa magari kwa
kiwango kikubwa katika jiji la Dar es
salaam.
Awamu ya
Tatu ya ujenzi itahusisha barabara za
Goba - Wazo hill -Tegeta Kibaoni (13.0Km), Mbezi Mwisho - Malambamawili- Kifuru
(6kM), Goba - Makongo ardhi (9km ) na Pia kukamilisha usanifu wa outering road
Bunju B - Mpiji Magohe - Victoria Kifuru hadi Pugu kiltex 33.7.
Wakala wa
Barabara nchini TANROADS unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara
katika jiji la Dar es salaam kwa kiwango cha lami ambapo barabara hizo
zinatarajiwa kuondoa tatizo la msongamano wa magari katika jiji hilo.
Post a Comment