Header Ads

Serikali kuwachukulia Hatua kali Watoa Huduma za Mawasiliano

Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano prof Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa kampuni za simu  nchini zilizo ingia makubaliano na serikali kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini  kukmilisha kazi hiyo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Prof.MBARAWA ametoa agizo hilo  mkoani IRINGA  mara baada ya kukagua  mitambo ya kampuni ya simu ya TTCL na kubaini kwamba bado kuna baadhi ya  vijiji havijafikiwa huduma ya mawasiliano  licha ya mkataba wa kutekeleza kazi hiyo  kati ya serikali na kampuni hizo kusainiwa miaka miwili iliyopita.

Tulikubaliana kwenye mkataba na tukawapa fedha  kwa ajili ya kupeleka mawasiliano vijijijni  hivyo ifikapo mwezi july kampuni yoyote ya simu itakayokuwa haijatimiza makubaliano hayo tutaipiga faini, Amesema prof. MABARAWA.

Kuhusu suala la kukatwa kwa mkongo wa taifawa mawasiliano  katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa IRINGA prof.MABAWA amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu au taasisi  itakayoharibu miundombinu hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) mkoa wa Iringa Eng. Ekael Manase akitoa taarifa ya Utendaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Watendaji wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoani Iringa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihakiki ujumbe wa Simu uliotumwa kwa mteja kumtahadharisha kuhusu zoezi la kuzima simu feki ,Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw,Richard Kasesela na Kushoto Meneja wa kampuni ya Simu (TTCL) Mkoa wa Iringa Eng.Ekael Manase.

No comments

Powered by Blogger.