Raia wa Kigeni 4792 Wakamatwa kwa Kukiuka Sheria za Uhamiaji
Frank
Mvungi-Maelezo
Takribani raia
4792 wakigeni wamekamatwa kwa kukiuka sheria,
Kanuni na Taratibu za Uhamiaji katika kipindi cha Januari hadi Aprili mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar essalam na Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abass Irovya wakati
wa mkutano na Vyombo vya habari uliolenga kutoa taarifa ya Operesheni mbalimbali
zinazotekelezwa na Idara hiyo.
Irovya amesema kuwa Idara hiyo imekuwa ikiendesha Operesheni
ondoa uhamiaji haramu tangu mwezi Desemba mwaka jana na imeonyesha mafanikio ambapo
raia1796 wamefukuzwa nchini kwa kukiuka sheria
za uhamiaji.
“Wananchi walio
wengi wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa Idara yetu kutokana na uelewa wao kuongezeka
kwa sababu tunayo program ya kutoa elimu
kwa umma na imeonyesha mafanikio makubwa”alisisitiza Irovya.
Bw. Irovya aliongeza
kuwa waliohukumiwa kifungo ni raia 132 na 383 kesi za o zinaendelea kwenye mahakama
katika Mikoa mbalimbali hapa nchini.
Raia 388
walilipa faini hali iliyochangia kuongeza mapato ya Serikali kutokana na kukiuka
sheria na Kanuni za Uhamiaji hapa nchini.
Kwa upande mwingine
kesi 509 zinaendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini na raia294 waliachiwa huru kutokana na mahakama kutowatia hatiani.
Idara ya
Uhamiaji ina Vituo takribani 60 katika Mikoa Mbalimbali hapa nchini baadhi vikiwa
katika Mikoa ya Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Katavi,
Kigoma, Simiyu ambapo Idara hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari
za raia wa kigeni wanaoingia nchini bila kufuata sheria na taratibu za Uhamiaji.
Post a Comment