Usaili wa Maisha Plus wafanyika Mkoani MTWARA
Ni asubuhi tulivu katika fukwe za bahari ya hindi kusini mwa Tanzania ambapo vijana wengi wamejitokeza kufanya usaili wa mashindano ya Maisha Plus East Africa 2016. Wapo wanaoonekana kujiamini na wengine wamejawa uoga. "Ni siku niliyoisubiri kwa hamu sana" anasema Faustine Komba miongoni mwa washiriki kutoka Mtwara.
Safari ya msimu wa tano wa mashindano ya Maisha Plus imeanza rasmi kwa kuanza na usaili uliofanyika katika hotel ya NAF Beach iliyoko Mtwara. Washiriki kutoka mikoa ya jirani nao pia walijitokeza. "Maisha Plus kwangu ni ndoto ya muda mrefu sana, niliposikia mnakuja Mtwara nikasema piga ua lazima nishiriki" Anasema Ismail Likando aliyesafiri kutoka Lindi.
Wakati usaili ukiendelea hali ya kujaa kwa maji baharini ilitokea na kulazimisha timu ya Maisha Plus kubadili utaratibu wa awali wa upigaji picha.
- Waandaaji wa mashindano ya Maisha Plus wakibadili utaratibu wa awali wa kupiga picha baada ya maji kujaa.
Muhitimu wa shahada ya kilimo William Mbaga alibanwa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo faida za kilimo cha 'greenhouse' pamoja na namna ambavyo maziwa ya mtindi yanapatikana,William alijieleza kwa ujasiri.
Washiriki wenye fani na ujuzi mbalimbali walijitokeza wakiwemo madereva bodaboda, mafundi, waigizaji, waimbaji, wasusi n.k
Post a Comment