Rais wa TFF Jamal Malinzi ampongeza Yussuf Manji
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amempongeza Yussuf Manji kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Young
Africans SC baada ya kupata kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa.
Kura mbili ziliharibika kwa nafasi hiyo
Kura mbili ziliharibika kwa nafasi hiyo
Kadhalika Rais Jamal Malinzi
amempongeza Clement Sanga kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti baada
ya kupata kura 1,428 wakati mpinzani wake Titus Osoro alipata kura 80.
Kura 1,508 zilipigwa katika nafasi ya kuwania makamu mwenyekiti.
Kadhalika wajumbe wanane
wanaounda Kamati ya Utendaji kwa kuchaguliwa kuongoza Klabu ya Young
Africans kwa miaka minne ijayo kwa mujibu wa katiba.
Wajumbe waliochaguliwa ni Omary
Said (1,069), Siza Lyimo (1,027), Salum Mkemi (894), Thobius
Lingalangala (889), Ayoub Nyenzi ((889), Samwel Lukumay (818), Hussein
Nyika (770) na Hashim Abdallah (727).
Katika salamu hizo za pongezi,
Rais Jamal Malinzi pia amewapongeza wanachama wa Young Africans kwa
kufanya uchaguzi wa amani na utulivu.
Kutokana na hali hiyo, Rais Jamal
Malinzi amewataka uongozi huo wa Young Africans kufungua ukurasa mpya
wa kuendesha klabu hiyo na kuiletea mafanikio klabu hiyo kongwe na
maarufu katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati hasa wakati
huu ambako Young Africans inashiriki hatua ya makundi ya Kombe la
Shirikisho Afrika (CAFCC).
Post a Comment