Header Ads

Waliomuua Simba CECIL kushtakiwa nchini ZIMBABWE

Picha kwa Hisani ya BBC
  .............................................

Wanaume wawili wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baadaye leo wakishtakiwa kwa makosa ya uwindaji , baada ya simba maarufu nchini humo kuuawa na mtalii mmoja raia wa Marekani .

Simba huyo,Cecil,alipigwa risasi nje kidogo ya mbuga ya wanyama ya taifa ya Hwange na Walter Palmer, daktari wa meno na mtu anayependa uwindaji Bwan Palmer -ambaye pia anaweza kukabiliwa na mashtaka , anasema anajuta kwa kumpiga risasi , lakini akasema alidhani alikua katika mawindo halali.

Maandamano juu ya kuuawa kwa simba huyo yamefanyika nje ya makaazi ya bwana Palmer katika jimbo la Minnesota nchini Marekani.

No comments

Powered by Blogger.