Header Ads

MWILI WA MMOJA WA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI YALIOVAMIA KITUO CHA POLISI STAKISHARI WAAGWA

Jeneza lenye mwili wa marehemu Koplo Gaudin Kakoko, likiwa  nyumbani kwa marehemu, Majohe, Ilala Jijini Dar es Salaam tayari kwa mwili wa marehemu kuagwa na wapendwa wake,Mwili huo ulisafirishwa jana kupelekwa kwao wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera kwa mazishi.Marehemu ni mmoja wa askari wanne waliouawa na majambazi hivi majuzi baada ya kukivamia kituo cha polisi Stakishari, Ukonga, Ilala Jijini Dar es Salaam, Mungu ailaze roho ya marehemu wote mahali pema peponi.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Majohe, Ilala Jijini Dar es Salaam tayari kuuaga mwili wa marehemu Koplo Kakoko amba0 ulisafirishwa jana kupelekwa kwao Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Ilala(SACP), Lucas Makondya akizungumza na waombolezaji kabla ya mwili huo kuagwa .
Sehemu ya waombolezaji wakimsikiliza Kamanda  Makondya. 
Baadhi ya askari waliohudhuria msiba huo wa kuuaga mwili wa mwenzao.
Jamaa wa karibu wa marehemu Koplo Kakoko wakijadili jambo, kushoto ni Filbert Katubazi na kulia ni Alvin Dogras .(Picha kwa hisani ya www.inocomm.blogspot.com)

No comments

Powered by Blogger.