Header Ads

KIONGOZI WA TALEBAN AHISIWA KUFARIKI DUNIA

Mullah Mohammed Omar, Kiongozi wa Taleban
Serikali ya Afghanistan inachunguza ripoti za kifo cha kiongozi wa kundi la Taliban, Mullah Mohammed Omar. Msemaji wa rais wa nchi hiyo ameyasema hayo kufuatia uvumi uliozagaa kuhusu kifo cha kiongozi huyo wa waasi. 

Wanamgambo wa Taliban wenyewe bado hawajatihibitisha rasmi kifo cha Mullah Omar, ambae hajaonekana hadharini tangu uvamizi wa majeshi yalioongozwa na Marekani 2001, ambayo yaliiondoa serikali ya Taliban mjini Kabulu.

Uvumi wa kuugua kwake, na hata taarifa za kifo zilitapakaa katika kipindi kilichopita. Ripoti ya hivi karibuni inatolewa siku mbili tu, kabla duru ya pili ya mazungumzo kati ya wanamgambo wa Taliban na serikali kufanyika.

Tangazo la msemaji wa rais, Sayed Zafar Hasheemi linatolewa kwa vyanzo ambavyo havikutambulishwa kutoka upande wa wapiganaji wa Taliban na serikali kuvieleza vyonzo vya habari, kikiwemo cha AFP kwamba kiongozi wa Taliban, alikuwa kapoteza uwezo wa kuona wa jicho moja kafariki dunia miaka miwili au mitatu iliyopita.

No comments

Powered by Blogger.