Header Ads

WAKILI ELIAS NAWERA ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KAWE JIJINI DAR ES SALAAM

Wakili Elias Nawera akionyesha alama ya dole baada ya kukabidhiwa fomu hizo. Kulia ni mgombea ubunge mkoa wa Dar es Salaam kupitia Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Lilian Mkosani.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe (kushoto), akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kawe, kada wa chama hicho, Wakili Elias Nawera (katikati), Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni mgombea ubunge mkoa wa Dar es Salaam kupitia Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Lilian Mkosani.
 Wakili Nawera (kulia), akiandika jambo kabla ya kulipa sh. 100,000  ya kuchukulia fomu.
 Hapa akimshukuru Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe baada ya kuchukua fomu hizo.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe (kushoto), akimuelekeza Wakili Elias Nawera mambo ambayo anapaswa kuyafuata baada ya kukabidhiwa fomu hizo.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni ambaye anamaliza muda wake Iddi Azani akimpongeza Wakili Nawera baada ya kuchukua fomu hizo. Azan alifika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake ya ubunge katika Jimbo hilo. 

No comments

Powered by Blogger.