ACT YAZUNGUMZIA MCHAKATO WA KUWAPATA WAGOMBEA WAKE
.
Baada ya chama cha Mapinduzi kupitisha majina matano kwenye tano bora ya Wagombea CCM nafasi ya Urais 2015 kupitia chama hicho.
Sasa kiongozi wa Chama Cha ACT 
Wazalendo, Mh Zitto Kabwe leo amefunguka kuhusu chama chake kumteua 
mgombea au kuunga mkono mgombea cha chama kingine.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter amewahabarisha wananchi kwa kusema…’Chama
 chetu kitateua mgombea au kuunga mkono mgombea wa chama kingine kwa 
maamuzi ya VIKAO vya chama. Kama Kiongozi wa chama sina mamlaka yeyote 
yale kutangaza mtu kuwa mgombea wetu’ – @zittokabwe
‘Hivi sasa
 Uongozi mzima wa Chama upo kwenye retreat ili kujipanga na uchaguzi. 
Hatuna mazungumzo wala makubaliano na mtu yeyote kutoka chama kingine 
kuhusu nafasi ya Urais. Mgombea wetu atapatikana kwa kupitia vikao vya 
chama chetu…’  -@zittokabwe
Post a Comment