Wateja wa SIMBA CEMENT kununua Saruji kwa Mfumo wa M PESA
Afisa
Mkuu Biashara wa Vodacom
Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba
Cement cha Tanga
(TTCL), Reinhardt Swart (kushoto) wakiwekea makubaliano ya mteja kunua saruji kwa M PESA bila
tozo yoyote popote
nchini.
Afisa Mkuu
Biashara wa
Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi kiwanda cha Saruji cha
Simba Cement Tanga (TTCL), Reinhardt (kushoto) wakibadilishana nyaraka za
makubaliano ya mteja kununua Saruji kwa M PESA bila tozo yoyote popote
nchini.
Afisa Mkuu
Biashara wa
Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) akizungumza mara baada makubaliano na
kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kwa mteja kununua Saruji kwa M PESA
bila tozo popote nchini.
Mmoja wa wakala wa Simba Cement Tanga, Athuman Ali (kulia) alievaa
kibagalashia akiwa mmoja wa watu waliohudhuria makubaliano ya utiaji
saini wa Ununuaji wa Saruji kwa M PESA baina ya Kampuni ya Vodacom
Tanzania na Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga leo.
William Mgazija wa ITV aliesimama nyuma na kushika MIC ni miongoni mwa
wahudhuriaji wa makubaliano ya utilianaji wa saini wa manunuzi ya Saruji
kwa M PESA.
Waandishi wa habari nao walikuwa miongoni mwa waalikwa wa ushuhudiaji wa
utilianaji saini makubaliano ya ununuzi wa Saruji kwa M PESA. Kutoka
kushoto alievaa Ushungi ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania , Betha
Mwambellah wa TBC na Maryam Mwandishi wa Jambo leo.
KIWANDA
Cha Saruji cha Simba Cement (TCCL) cha Tanga, kimeinmgia makubaliano
na Kampuni ya
simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania Limited, kwa mteja kununua saruji kwa
kutumia M PESA bila tozo yoyote.
Makubaliano hayo
yaliyofanyika leo
viwanja vya Hotel ya Tanga Beach na kushuhudiwa na viongozi wa pande zote mbili
na kutajwa kuwa yatakuwa mkombozi kwa mwananchi wa kipato cha chini kwa kununua
Saruji kwa simu badala ya kutumia Taasisi za pesa na kupanga
foleni.
Akizungumza na
waandishi wa habari,
Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond, alisema kampuni yake
imechukua uamuzi huo wa makubaliano na kampuni ya Cement kwa lengo la kumsaidia
mwananchi wa kipato cha chini.
Alisema mteja ataweza
kununua Saruji
(Simba Cement) kwa kutumia M PESA na hakutakuwa
na tofati ya mnunuzi wa mifuko mingi na michache ambapo hatotozwa ada yoyote
mnunuaji.
Kwa upande wake,
Mkurugenzi wa
kiwanda cha Saruji, Simba Cement, Renhardt Swart, alisema makubaliano hayo ni
moja ya sera za kiwanda kumsaidia mwananchi wa chini kuweza kukabiliana na
changamoto za maisha.
Alisema Kiwanda cha
Simba Cement
daima kiko kwa ajili ya wananchi na faida inayopata inairejesha kwa wananchi na
kuwataka kuitumia fursa hiyo ambayo iko na unafuu kwa
ununuaji.
Post a Comment