Benki Kuu ya TANZANIA yashauriwa Kufanya Utafiti Kuhusu Ununuzi wa Mazao
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika kwa engo la kujitabulisha. |
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakimsikiliza kwa makini Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo June 28 mwaka huu. |
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakiwa makini katika mkutano huo. |
Mgeni rasmi katika picha ya Pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki hiyo. |
Na
EmanuelMadafa
SERIKALI
MKOANI Mbeya imeitaka benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya kufanya utatifi juu ya kuwepo kwa ununuzi wa
mazao kwa wakulima mapema kabla ya kuanza kukomaa hususani mazao ya ndinzi hasa
katika halmsahuri ya wilaya ya Rungwe Mkoani humo.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla wakati akizungumza na wafanyakazi wa benki Kuu Tanzania (BOT)tawi
la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo yenye lengo la
kujitambulisha.
Amesema kwa
muda mrefu sasa wakulima wa mkoa huo
wamekuwa wakinyonywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakinunua mazao
mapema yakiwa shambani na kupangia bei ya chini ambayo haiendani na bei hali ya
sokoni.
Amesema nivema benki hiyo ikajaribu kulifanyia
utatiti suala hilo ili kuona kama mfumo
huo unaweza kuleta tija kwa mkulima kwani benki hiyo inanafasi nzuri ya kuisaidia
serikali katika uchocheaji wa ukuaji wa uchumi.
Amesema
lengo la serikali ni kuwalinda wananchi wake sanjali na kuwaondolea umaskini
hivyo lazima ifanyike kila aina ya jitihada katika kufanikisha suala hilo.
Wakati huo
huo Mkuu huyo wa Mkoa wa mbeya Amosi Makalla ameipongeza benki hiyo kwa kuweka
jitihada za makusudi katika kudhibiti mfumuko wa bei nchini.
Amesema kama
mfumuko wa bei utashindwa kudhibitiwa tafsiri halisi ya kukua kwa uchumi
haitakuwa na maana yeyote kwa mwananchi wa kawaida hivyo lazima benki hiyo
ikaongeza jitihada zaidi katika kudhibiti hali hiyo.
Kwa upande
Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania( BOT)tawi
la Mbeya Ndugu Juvent Rushaka amesema benki hiyo iko tayari kufanya utafiti suala
lolote la kiuchumi.
Aidha
Mkurugenzi huyo ameelezea changamoto mbalimbali ambazo tawi hilo linakutana
nazo likiwemo suala la kutopata takwimu
mbalimbali kwa usahihi na kwa wakati.
Amesema
changamoto nyingine ni miundombinu ya kiusalama ya majanga ya moto kwa kipindi
kirefu sasa kwa ukosefu wa maji katika bomba la kuzimia moto hali ambayo ni
hatarishi endapo litatokea janga la moto katika twi hilo .
Post a Comment