Waziri
wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwibara, iliyopo katika Jimbo hilo,
mara baada ya kuzindua ugawaji wa vitabu zaidi ya 22,000 katika Shule za Msingi
na Sekondari za Jimbo la Musoma vijijini. Maboksi yanayoonekana ni ya baadhi ya
vitabu hivyo vinavyosambazwa katika Jimbo hilo.
“Nimeleta
rafiki zangu kutoka China na watawatibu kwa muda wa siku Mbili lakini pia
Madaktari hawa wanaojitolea wamekuja na rafiki zao ambao wameleta, kalamu na
vitabu vya Sayansi, Hisabati, na Kiswahili, kwa ajili ya kugawa katika shule
Tano za Msingi, pamoja na mipira ambayo itagaiwa katika shule hizo na timu za
mipira za hapa kijijini,” alisema Profesa Muhongo.
Naye
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa China hapa nchini, Bwana Zhang Biao, alisema kuwa
uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi za Tanzania na China ndiyo umechangia kwa
kiasi Madaktari hao kutoka China kuja nchini kutoa huduma hizo za matibabu.
“Ushirikiano
wetu unazidi kupanuka na wanachi wengi wa China wanakuja Tanzania kufanya
biashara, hali kadhalika wananchi wa Tanzania wanaenda China kwa masuala ya
Bishara na Utalii, kwa ushirikiano huu tutazidi kupanuka hata kiuchumi,”
alisema Zhang.
Alisema
kuwa hadi sasa kuna Madaktari zaidi ya 20 kutoka China wanaotoa huduma za
matibabu nchini ambao wapo katika mikoa ya Dar es Salaam, Tabora, Mara na
Dodoma na hii yote inatokana na urafiki na undugu uliopo katika ya nchi hizo
mbili.
Wakati
huohuo Profesa Muhongo amezindua ugawaji wa vitabu zaidi ya 22,000 katika Shule
za Msingi na Sekondari za Jimbo la Musoma vijijini ambapo uzinduzi huo
ameufanya katika shule ya msingi Kwibara kata ya Mugango.
Katika
uzinduzi huo, Profesa Muhongo alisema kuwa Jimbo hilo lina shule za msingi 108
na Sekondari 20 ambapo kila shule ya msingi itapata maboksi ya vitabu mawili
huku kila shule ya sekondari ikipata maboksi 16.
Profesa
Muhongo alisema kuwa vitabu hivyo ameletewa na Rafiki zake kutoka nchini
Marekani ambapo thamani ya vitabu hivyo ni Dola za Marekani 250,000, “ lengo
langu ni kuhakikisha kuwa wananchi katika Jimbo hili mnaelimika kwa kujenga
utamaduni wa kujisomea, hivyo vitabu hivi hata wananchi mnakaribishwa kuja
kuvisoma,”alisema Profesa Muhongo.
Aidha,
Profesa Muhongo alisema kuwa katika kutimiza ahadi zake,
amewapeleka wananchi hao Gari aina ya Canter Kwa ajili ya kusaidia katika
Shughuli za Misiba, ujenzi wa Shule, Maabara na vituo Vya Afya, pia ametimiza ahadi ya gari ya kubebea
wagonjwa ambapo mwezi Machi, 2016 alilikabidhi Gari hilo la wagonjwa katika
Hospitali ya Murangi.
Akiwaeleza
wananchi Mipango ya kuendeleza huduma za Afya katika Jimbo la Musoma Vijijini,
alisema kuwa " Leo nawataarifu kuwa baada ya wiki 2 nitaleta gari nyingine
4 za kubebea wagonjwa na zitagawanywa katika Zahanati ya Kurugee, -Kata ya Bukumi, Zahanati ya Masinono-Kata ya Bugwema,
Zahanati ya Mugango-Kata ya Mugango na Zahanati ya Nyakatende-Kata ya
Ifulifu.
Vilevile
alisema kuwa bado kuna vitabu vingine vinavyoendelea kuletwa nchini ambapo Awamu
nyingine ya 3 inategemewa kufika Mwezi Agosti, 2016 ambavyo pia atavigawa
katika Majimbo mengine ya Mkoa wa Mara bila kubagua itikadi ya Chama kwani
wananchi wote wana haki ya kupata maendeleo, aidha Awamu ya 4 ya vitabu
inategemewa kufika mwezi Octoba, 2016.
|
Post a Comment