Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wageni mbalimbali mara baada ya kupokea
Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi(NEC) Jaji Damian Lubuva
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya
upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Uchaguzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
mwanasiasa mkongwe John Shibuda huku Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Dkt. Ali Mohamed Shein naye akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee
John Momose Cheyo mara baada ya kukamilika kwa tukio la upokeaji wa Taarifa ya
Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Baadhi
ya Wageni na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wimbo wa
Taifa ukipigwa kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kupokea taarifa hiyo ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC).
Post a Comment