Serikali yaonya Juu ya Matumizi Mabaya ya Vyandarua
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Mpoki Ulisubisya akikata utepe kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya
Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es
salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Mpoki Ulisubisya akizungumza na wadau mbalimbali wa takwimu hawapo
pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya
Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Mpoki Ulisubisya akionyesha kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya
Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 kwa wadau wakati wa uzinduzi
huo leo jijini Dar es salaam.
Wadau
mbalimbali wa takwimu wakifauatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha
Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16
leo jijini Dar es salaam.
Na Ally Daud-Maelezo
SERIKALI imetoa wito kwa wananchi
kuacha matumizi mabaya ya vyandarua ili kusaidia jitihada za Serikali
katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.
Akizungumza leo Jijini Dar es
salaam katika Uzinduzi wa Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto
na Malaria wa Mwaka 2015/16, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa
kumekuwepo na tabia ya wananchi kutumia vyandarua wanavyopewa na
Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi kama kuvulia samaki, kuwekea wigo
mifugo na kuzungushia wigo bustani.
‘‘Watu wengi wamekuwa wakitumia
vyandarua vinavyotolewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi badala ya
kujikinga na Mbu waenezao malaria. Hii ni kutokana na utafiti huu
kuonyesha kuwa asilimia 14 ya watoto wa chini ya miaka 5 ambao walipimwa
Malaria kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid
Diagnostic Tests (RDT) walikuwa na Malaria,” amesema Dkt. Ulisubisya.
Aidha amesema kuwa kiwango cha
maambukizi ya Malaria bado ni kikubwa ikilinganishwa na kiwango
kilichopatikana wakati wa Utafiti wa UKIMWI na Malaria wa Mwaka 2011-12
hivyo ni vyema jamii ikaendelea kupambana na ugonjwa huu kwani bado ni
tishio kwa watoto na Wananchi kwa ujumla.
Dkt. Ulisubisya amesema
kuzinduliwa kwa Matokeo haya kutasaidia Serikali kuboresha huduma za
afya kwa kuyafanyia marekebisho mapungufu yaliyopo katika utoaji wa
huduma za malaria nchini.
Akizungmzia huduma za afya kwa
akinamama wajawazito, Dkt. Ulisubisya amesema utafiti umeonyesha kuwa
kiwango cha akina mama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma
ya afya, kutoka asilimia 51 mwaka 2010 kufikia asilimia 60 mwaka 2015 na
kuongezeka kwa kiwango cha akina mama wanaosaidiwa na wataalam
waliosomea wakati wa kujifungua kutoka asilimia 50 kufikia asilimia 60
mwaka 20015/16.
Akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Shughuli za Kitakwimu, Mr. Irenius Ruyobya amesema kuwa utafiti huu
ni wa muhimu sana katika kuboresha huduma za afya hasa katika kupambana
na Malaria.
Amesema ili Serikali iweze
kuboresha huduma za afya na kupambana na Malaria, takwimu hizi ambazo
zimezinduliwa leo zitasaidia Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa afya
katika kupanga, kutekeleza na kupima utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya afya nchini.
Mr. Ruyobya amesema utafiti huu
ni wa sita kufanyika nchini ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka
1991 na kufuatiwa na utafiti wa mwaka 1996, 1999, 2004/5 na 2010.
Post a Comment