Wanawe Rais KAGAME waichezea timu ya Rwanda
Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 katika mechi ya kuadhimisha miaka 22 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
Mchuano huo wa kumbukumbu, kati ya Rwanda na Morocco ulioandaliwa katika uwanja wa Amahoro, mjini Kigali ulikamilika kwa sare ya goli moja.
Ingawa wote wawili hawakukamilisha mechi hiyo. Kocha wa Rwanda Kayiranga Jean Baptista aliwapa nafasi ikiwa ni mechi yao ya kwanza kuvaa sare ya timu ya taifa ya soka.
Ian Kigenza Kagame alijumuishwa katika kikosi kilichoanza kabla ya kumpisha Park Udahemuka kunako dakika ya 27.
Rwanda maarufu nyigu wachanga walitangulia katika dakika ya kwanza kupitia Blaise Itangishaka.
Hata hivyo Morocco ilisawazisha katika dakika ya 43 baada ya Morocco Dari Achraf kumuandalia krosi Hicham Boussoufiane.
Kunako dakika ya 74, Kitinda mimba wa familia ya kagame, Bryan Kagame alichukua nafasi yake Djabel Manishimwe.
Baba yao wawili hao, Rais Paul Kagame ni shabiki wa soka na tenisi na ni shabiki sugu wa klabu ya Arsenal ya Uingereza.
Post a Comment