Mamlaka ya Elimu TANZANIA yapongeza Kwa Kuinua Sekta ya Elimu Nchini
Na
Hassan Silayo
Aliyekuwa
Mkuu wa Wilaya ya Same Herman Kapufi ameshukuru Jitihada zinazofanywa na Mamlaka
ya Elimu Tanzania (TEA) katika kutekeleza miradi inayosaidia kuongeza ubora wa
elimu nchini.
Ikiwemo utekelezaji wa mradi kukarabati shule kongwe nchini utakaoboresha
mazingira ya kufundishia na kusaidia kuinua kiwango cha elimu katika shule
hizo.
Mh.
Kapufi amesema kuwa mpango huo umekuja wakati muafaka wakati uongozi wa wilaya
hiyo ukipambana kutatua changamoto za elimu na kuwataka wadau kuipa ushirikiano
Mamlaka hiyo.
“Kwa
kweli napenda kuishukuru Mamlaka ya elimu Tanzania kwa jitihada zake hizi za
kuboresha sekta ya elimu nchini, kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana katika
wilaya hii kwa kipindi chote nilichokuwa hapa kama mkuu wa wilaya, shule zetu
kongwe zimechoka sana na zinahitaji ukarabati ili kuweza kuzirudisha katika
hali yake ya kawaida kwa utekelezaji wa mpango huu” Alisema Mh.Kapufi.
Naye
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bibi. Sylvia
Lupembe amesema kuwa kupitia TEA mpango huo utatekelezwa katika shule kongwe 11
katika mikoa ya Bukoba, Mwanza, Tabora, Singida, Same, Arusha, Dodoma, Morogoro
na Pwani kwa kuzifanyia ukarabati wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo madarasa, vyoo,
maabara, mabweni na mifumo ya umeme.
“hali
ya shule zetu kongwe kwa kweli sio nzuri tumetembea kwenye mikoa takribani
Mikoa sita tumejionea halihalisi ya miundombinu ya shule zetu kongwe hazipo
katika mazingira mazuri ya kujifunzia kutokana na kuwa na miundombinu chakavu
na kwa mradi huu tunataka kuweka mazingira mazuri ya watoto wetu hawa
kujifunzia hasa kwa kuanza na shule hizi kongwe” Alisema Sylvia.
Wakizungumzia
ukarabati huo Mwalimu Mkuu wa shule wa Shule ya Sekondari Nganza Bi. Yacinta
Lyimo aliishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa Utekelezaji wa mpango huo
kwani utasaidia kuboresha mazingira ya kufundishia na hata kusaidia kuinua kiwango
cha elimu na ufaulu katika shule hizo.
Aidha,
Afisa Elimu wa Manispaa ya Singida Bw. Omari Kisuda Mpango huu wa maboresho ya
shule kongwe ni mkombozi katika sekta ya elimu na umekuja wakati uhitaji wa
maboresho ya shule hizo unahitajika hasa kutokana na baadhi ya shule kushindwa
kufanya ukarabati wa mara kwa mara kutokana na ufinyu wa bajeti.
Post a Comment