Umeme Vijijini Kuwatoa WATANZANIA katika Umasikini
Injini ya kuinua uchumi wa
Tanzania kutoka uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati imetajwa kuwa ni
uwepo wa umeme wa uhakika unaoendana na mahitaji.
Hayo yamesemwa leo, mjini Dodoma
na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo alipokuwa
akijibu hoja mbalimabli za Wabunge zinazohusu upataikanaji wa nishati ya
umeme.
“Bajeti ya mwaka 2016/17
itahakikisha umeme unapatikana vijijini ambapo Wizara ya Nishati na
Madini katika bajeti hii imeongezewa asilimia 50 zaidi ya bajeti
inayoisha ya mwaka 2015/2016, ili kuhakikisha umeme unapatikana
Vijijini,” alisema Mhe. Muhongo.
Mhe. Muhongo aliendelea kusema
kuwa, bajeti hiyo inahakikishha vyanzo vyote vya umeme kama vile gesi
asilia, upepo, mawimbi, makaa ya mawe, jotoardhi na jua vinazalisha
umeme Nchi nzima.
Aidha, Waziri huyo amesema kuwa
bajeti hiyo itapelekea kuboreshwa kwa upatikanaji wa umeme kwa kupitia
sheria na taratibu zinazoipa mamlaka TANESCO peke yake kutoa huduma ya
umeme kwa kuleta ushindani katika kutoa na kusambaza umeme Nchini.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah Kairuki akijibu hoja kuhusu swala la kuwepo kwa watumishi hewa
na hatua zinazochukuliwa kukomesha tatizo hilo, amesema kuwa Serikali
iko tayari kufukuza Maafisa Utumishi wote ambao wamesababisha kuwepo kwa
watumishi hewa ili kubaki na Maafisa Utumishi ambao ni wazalendo,
waadilifu na wachapakazi.
Post a Comment