Header Ads

Tigo Pesa yatoa Fursa ya Biashara Kwa Wajasiriamali

Mkuu wa Huduma za Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Makumbusho Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu Tigo Pesa kutoa fursa za biashara kwa wajasiriamali. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa Tigo, Temitope Ayedum na kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.

Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale 

 WAJASIRIAMALI wa kidijitali pamoja na wabunifu wa matumizi ya simu Tanzania hivi sasa wanaweza kuleta ufumbuzi zaidi kwa mteja katika soko na kuongeza  shughuli zao za kibiashara  kupitia  jukwaa  la huduma za kifedha kwa simu la Tigo Pesa.
Tigo Pesa ambayo inaongoza Tanzania kwa kutoa  huduma za kifedha kwa njia ya simu imefuatilia  uhusiano wake wa karibu na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuanzisha programu ambazo zinatoa mwongozo wa hatua kwa hatua  kwa wajasiliamali wa kijitali kwa kuiunganisha Tigo Pesa katika matumizi yao. Hatua hiyo inajionesha katika wavuti wa www.tigo.co.tz.

 Akizungumza katika mkutano na waandioshi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Huduma za Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel alisema, “Tigo imewekeza  zaidi ya dola milioni 15 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita  katika kuboresha jukwaa la ngazi ya kimataifa  na huduma  ili kuendelea  kutoa  huduma sahihi za uhakika, zinazofikiwa na salama  kwa wateja.”
Swanepoel  alifafanua:“Jukwaa hilo la kuwanunganisha wateja wa Tigo Pesa na mitandao mingine  kwa kiwango kikubwa itapunguza  changamoto ambazo wajasiriamali wanakumbana nazo  katika kuunganisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika kupokea malipo  kutoka kwa wateja wake katika hali isiyo na hitilafu na hivyo kuongeza  wigo jumuishi kifedha kote nchini.”
Swanepoel  aliongeza kwamba, “Tigo pesa imejikita kuangalia  hali na uwezo wa kuwezesha maendeleo ya  huduma za ubunifu na kujumuisha bila tatizo mitandao mingine  ili kuwapa wateja  faida zaidi za huduma ya fedha kwa njia ya simu.”
Itakumbukwa kwamba kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2016, Tigo Pesa  ilikamilisha  ushirikiano wake na  watoaji wengine wa huduma za fedha kwa njia ya simu  na benki nchini  kwa kuzifanya huduma hizo kupatikana kwa watu wengi zaidi.  Tigo Pesa pia ilizindua kifaa cha wateja kwa Android kwa watumiaji IOS, kwa kuwapatia njia rahisi watumiaji pindi wanapotumia  huduma zake.
Mfumo wa kuendesha na kutumia program hii ijulikanayo kama ‘Application Program Interface (API)  ni muundo wa maelekezo  na viwango vya kufikia mtandao  kwa kutumia zana  za kompyuta au zana za kimtandao. Ili kuzifikia programu za Tigo Pesa  inamaanisha wanafunzi wa vyuo, wajasiriamali wa biashara elektroniki , wabunifu wa vifaa  na wataalamu wengine wa teknolojia ya habari  wanaweza kuibuka na  vifaa  au kuwezesha  vifaa vilivyopo  kwa kuunganisha  ufumbuzi wao na Tigo Pesa.


No comments

Powered by Blogger.