Makamu wa Rais SAMIA SULUHU afungua Mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiriamali yalioandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mhe. Mama Anna Mkapa akihutubia kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ambapo mgeni Rasmi wa ufunguzi huo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Ndugu Steven Martin akielezea kwa ufupi mafanikio ya mafunzo ambayo yametimiza miaka 19.
Sehemu ya wakina ama waliohudhuria ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani,Dar Es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Esther Mkwizu akizungumza na wajumbe walihudhuria mara baada ya unfunguzi rasmi wa mafunzo kufanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janetth Magufuli ,Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema wakifurahia jambo wakati wa shughuli za ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali wanawake ,kushoto ni Mwenyekiti wa wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
Baadhi ya wakina Mama waliohudhuria wakifuatilia kwa makini hotuba za ufunguzi wa mafunzo ya wanawake wajasiriamali.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Jacline Maleko akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Wanawake Wajasiriamali yaliofanyika kwenye Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.
Post a Comment