Na
Devota Myombe
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania,
Egon Kochanke pamoja na Balozi wa Denmark nchini, Einar Jensen kujadili ujenzi
wa Kiwanda cha mbolea wilayani Kilwa.
Katika mkutano huo,
ilielezwa kuwa matayarisho ya ujenzi wa kiwanda hicho cha mbolea chenye thamani
ya Dola za Marekani bilioni 1.5 yanaendelea na kwamba kiwanda hicho
kinatarajiwa kuzalisha tani milioni 1.35 za mbolea kwa mwaka.
Waziri Muhongo
alisema ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho ipo na kuwa gesi asilia
itakayotumika kiwandani hapo ipo ya kutosha.
Alisema kampuni
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zitakuwa na hisa katika kiwanda hicho
ambapo kwa upande wa Tanzania, alizitaja kampuni hizo kuwa ni Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Minjingu Mines pamoja na Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
|
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza kwenye kikao na mabalozi kutoka
Ujerumani na Denmark (hawapo pichani) hivi karibuni katika Ukumbi wa Wizara
jijini Dar es Salaam.
|
|
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo(Kulia) akijadiliana jambo na Balozi wa
Denmark, Einar Jensen (Kushoto). Katikati ni Balozi wa Ujerumani, Egon Kochanke
akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni ofisini kwa Waziri jijini Dar es Salaam
hivi karibuni.
|
|
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo(Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi
wa Ujerumani, Egon Kochanke(Kulia) na Balozi wa Denmark, Einar Jensen(Kushoto).
Aidha, kwa upande wa
kampuni za nje, Profesa Muhongo alizitaja kuwa ni Ferrostaal ya Ujerumani,
Haldor Topsoe ya Denmark na Fauji kutoka nchini Pakistan.
Profesa Muhongo
aliwahakikishia mabalozi hao pamoja na ujumbe wao kuwa ardhi kwa ajili ya
uwekezaji wa kiwanda hicho ipo na kwamba gesi asilia itakayohitajika ipo ya
kutosha na kuwa bado nafasi za uwekezaji zinapatikana. “Ardhi ipo, gesi ipo
hivyo mnakaribishwa,” alisema Prof. Muhongo.
Naye Balozi wa Ujerumani
nchini, Egon Kochanke alimshukuru Profesa Muhongo kwa kukubali kukutana na
ujumbe huo kupokea maombi ya mpango wa ujenzi wa Kiwanda hicho cha mbolea
ambapo alisema, hiyo ni njia mojawapo ya kuboresha uzalishaji Tanzania.
“Nimefurahi sana kushiriki kikao hiki na nina kushukuru kwa kukubali kwako kupokea
maombi haya,” alisema.
Kwa upande wake
Balozi Einar Jensen alitumia nafasi hiyo kumshukuru Profesa Muhongo kwa jinsi
alivyoupokea ujumbe huo na namna alivyoendesha majadiliano husika.
Kikao hicho pia
kilihudhuriwa na baadhi ya watendaji wa Wizara pamoja na taasisi zilizo chini
ya Wizara ya Nishati na Madini.
|
Post a Comment