Bilioni 2.5 Kuanza kujenga Hospitali ya Wilaya ya MOROGORO
Hayo yamesemwa leo,Mjini Dodoma
na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Selemani Jaffo alipokuwa akijibu
swali la Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Azizi Abood juu ya msongamano
mkubwa wodi za akina mama hospitali ya Rufaa Morogoro.
“Msongamano wa wagonjwa katika
wodi ya wazazi Hospitali ya Mkoa unatokana na kukosekana kwa hospitali
ya Wilaya ya Morogoro.Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali immepanga
kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Morogoro katika bajeti ya mwaka
2016/17,” alisema Mhe. Jaffo.
Mhe. Jaffo aliendelea kusema
kuwa, fedha hizo zilizotengwa zitaanza kwa ujenzi wa jengo la utawala na
jengo la wagonjwa wa nje.(OPD).
Aidha, aliendelea kujibu maswali
ya yaliyoelekezwa katika wizara hiyo kwa kusema kuwa, Serikali katika
bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi
wa chumba cha kuhifadhi maiti (mortuary) Wilaya ya Chunya.
Chumba hicho cha kuhifadhi maiti
kinatarajiwa kugharimu shilingi milioni 230 ambapo ujenzi wa jengo
utagharimu shilingi milioni 60 na Majokofu yatagharimu shilingi milioni
160.
Kwa sasa Wilaya hiyo ina chumba
maalum ambacho kimetengwa kwa ajili ya kuhifadhi mati mbili tu ambacho
hakitoshelezi huduma hiyo hali ambayo huwalazimu wahitaji kufuata huduma
ya kuhifadhi maiti Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
Post a Comment