WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MATHIAS CHIKAWE, AZINDUA HUDUMA ZA “DUTY FREE SHOP” GEREZA KUU LILUNGU, MKOANI MTWARA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(kulia) akifurahia
kwenye jiwe la Msingi mara tu baada ya kuzindua rasmi duka hilo lenye
bidhaa zisizo na tozo la Kodi(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) ni Mkurugenzi wa
Transit Military Shop, Bw. Alfazar Meghji. Uzinduzi huo umefanyika Julai
5, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara.
Bidhaa
mbalimbali zinazopatikana katika Magereza “Duty Free Shop” ya Gereza
Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara kama inavyoonekana katika picha. Duka hilo
limezinduliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias
Chikawe(hayupo pichani).
Muonekano wa nje wa Magereza “Duty Free shop” ya Gereza Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara kabla ya kuzinduliwa rasmi leo Julai 5, 2015.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi ya
uzinduzi wa Magereza “Duty Free Shop” Gereza Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara
leo Julai 5, 2015 katika Viwanja vya Lilungu, Mkoani Mtwara.
Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereeza kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa
Magereza “Duty Free Shop” Gereza Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja(kulia) akiteta jambo na
Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe. Christopher Magala(kushoto) kwenye hafla
ya ufunguzi rasmi wa Magereza “Duty Free Shop Gereza Kuu Lilungu, Mkoani
Mtwara.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa
ya Lindi na Mtwara kwenye uzinduzi wa Magereza “Duty Free Shop” Gereza
Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara(wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa
Magereza, John Casmir Minja(wa tano kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani
Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mussa Kaswaka(wa pili kushoto)
Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe. Christopher Magala(wa kwanza kushoto) ni
Mkurugenzi wa Transit Military Shop, Alfazar Meghji.
……………………………………………………………………
Na, Lucas Mboje, Mtwara
Maafisa na Askari wa Jeshi la
Magereza nchini wametakiwa kutumia fursa ya maduka yenye bidhaa nafuu
“Duty Free Shop” zilizofunguliwa katika Magereza mbalimbali ili kupata
vifaa vya ujenzi na kujenga makazi yaliyobora na ya kudumu kabla ya
kustaafu Utumishi wao Jeshini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe alipokuwa akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa Magereza “Duty Free Shop” ya Gereza Kuu
Lilungu, Mkoani Mtwara.
Amesema kuwa Maafisa na Askari
wakitumia vizuri fursa ya maduka haya kwa kununua bidhaa za vifaa vya
ujenzi itasaidia kukwepa aibu inayowapata baadhi ya Maafisa na Askari
baada ya kustaafu hivyo kukosa nyumba za kuishi wakitegemea kujenga kwa
kutumia Mafao baada ya kustaafu.
“Serikali iliidhinisha
utaratibu wa Maafisa na askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama
kusogezewa Huduma hizo za bidhaa muhimu katika maeneo yao kwa gharama
nafuu kwa lengo la kuwapunguzia makali ya maisha”. Alisema Waziri
Chikawe.
Kwa upande wake Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja amesema kuwa Jeshi la Magereza
limejipanga kuhakikisha kuwa linasambaza huduma hizo nchi nzima kwa
ajili ya kutoa huduma kwa Maafisa na askari nchini.
Hadi sasa Jeshi hilo limekwisha
kuzindua “Duty Free Shops” Nane katika Mikoa ifuatayo Dar es Salaam –
Ukonga na Keko, Mwanza – Butimba, Tabora – Uyui, Kingolwira – Morogoro,
Mbeya – Ruanda, Dodoma – Isanga na Mtwara – Lilungu.
Post a Comment