SOKO LA SINZA BUS TERMINAL LAZINDULIWA RASMI
Meya wa manispaa ya Kinondoni
Yusufu Mwenda akiwa na watendaji wa soko hilo akizungumza mara baada ya
kukagua vizimba vyo soko hilo kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika zunduzi huyo.
………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
MSTAHIKI Meya wa manispaa ya
Kinondoni, Yusufu Mwenda amesema kuwa soko jipya la SIMU 2000 litaweza
kuchukua wafanyabiashara 512 kutoka kila pembe ya manispaa ya kinondoni.
Mwenda amewatoa hofu
wafanyabiashara wa soko jipya la kituo cha basi cha Simu2000
mawasiliano kuwa watafanya biashara bila ya kuwa na matatizo yoyote kwa
kuwa soko hilo lipo katika mfumo wa kisasa.
Mwenda alisema hayo alipokuwa
akikabidhi vizimba vya soko hilo kwa wafanya biashara ndondogo waishio
katika wilaya ya kinondoni na sio mtu kutoka eneo la nje ya manispaa
hiyo hivyo kuwataka kulitunza soko hilo kama mali yao.
“tumeamua kulifanya soko hili
hili liweze kuanza kazi kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanywa baadae hili
kuweza kuwapa fursa wafanya biashara kuliko kuacha jingo limeisha na
kuonekana kama picha hivyo nawaomba mfanye biashara hili muweze
kujiongeza kipato” alisema Mwenda.
Alitoa wito kwa wafanyabiashara
hao kutokata tamaa kwani mwanzo ni mgumu kwani eneo lenyewe ni jipya
hivyo sio rahisi kuona biashara ikichanganya kwa haraka kama
wanavyofikiri.
Mstahiki Meya aliwataka wafanyabiashara hao kuanza biashara mara moja ili kutimiza lengo la kujengwa kwa soko hilo.
Mmoja wa wafanyabiashara
ndogondogo aliyepata nafasi katika soko hilo aliishukuru manispaa ya
Kinondoni kwa kuona umuhimu wa kujenga soko hilo, kwani pamoja na
kuwaongezea wao vipato kwa kufanya biashara pia itasogeza huduma karibu
hata kwa abiria na majirani wa kituo hicho cha Sinza Bus Terminal.
Post a Comment