RAIS JAKAYA KIKWETE, AJIANDIKISHA KUPIGA KURA KWA MFUMO WA BVR, KIJIJI KWAKE MSOGA
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo
mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha
Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.Kulia akiangalia kwa makini ni
mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa
TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto
aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.
Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume
ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za
vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda
kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo leo.
Bwana SANIF Khalfan ambaye ni
Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha
kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga
leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko
kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Mwenyekiti wa tume ya Taifa
ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimpngeza Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete baada ya kumkabidhi kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya
Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia
teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
(picha na
Freddy Maro)
Post a Comment