NHC YANYANG’ANYA MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI, BAADA YA HALMASHAURI ZA MIKOA KUSHINDWA KUTUMIA FURSA HIYO
● Mkoa wa Katavi na Rukwa washindwa kutumia fursa ya msaada huo
● NHC yanyang’anya mashine Halmashauri za Mikoa hiyo
● Zatakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara
...............................................
...............................................
Katika kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatunzwa, kutumika
ipasavyo na kuhakikiwa, NHC imeendelea kuwakagua vijana waliopewa
msaada wa mashine za kufyatulia matofali yatakayowezesha wananchi
kujijengea nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri zote za Mikoa ya
Katavi, Mbeya na kukamilika Mkoani Iringa.
Kwa ujumla, vijana wana ari
ya kutosha ingawa wana changamoto zinazohitaji msukumo wa Halmashauri
zao, hasa za masoko ya matofali yao pamoja na mtaji wa kuwawezesha
kuendelea na uzalishaji wa benki ya matofali ya kuuzia wananchi.
Katika
ziara ya NHC Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya hizo wameomba NHC
isiwanyang’anye mashine na wameahidi kuwapa vijana mikopo na kuwasaidia
malighafi za kuwawezesha kutengezea matofali hayo ikiwemo mchanga,
sementi na udongo maalum kwa kazi hiyo.
Hata hivyo, Mikoa ya Rukwa na
Katavi muitikio wa vijana na Halmashauri hizo ukiacha Halmashauri ya
Mlele ambayo inafanya vizuri, umekuwa hafifu sana na Shirika
limelazimika kuzinyang’anya Halmashauri hizo mashine na kuzitaka kuomba
upya kama bado wana azma ya kutumia mashine hizo kujiletea maendeleo ya
kuwa na nyumba bora na kukuza ajira kwa vijana wao.
Fuatilia yaliyojiri
katika uhakiki huo katika picha hapa chini....
Kikundi cha ‘Mshikamano’
katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kikimsikiliza Meneja wa Huduma kwa
Jamii wa NHC BW. Muungano Saguya akiwaelezea namna ya kukuza ujuzi na
kutumia Halmashauri zao kuongeza ufanisi wa kazi alipowatembelea
nakusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili, Vijana hao wameshapewa
eneo la muda la kuendesheea shughuli zao na wameanza kutengeneza tofali
kwa ajili ya kuwauzia wananchi.
Hii ndiyo hali iliyojitokeza
Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda pale NHC
ilipolazimika kuzitwaa mashine ilizotoa msaada kwa vijana ili waweze
kujiajiri, Kikundi hiki cha Mpanda Hotel ni mojawapo ya vikundi
vilivyonyang’anywa mashine Mkoani Katavi na Rukwa kwa Halmashauri sita
za Mikoa hiyo ukiacha Mlele inayofanya vizuri, kushindwa kuzitumia
mashine hizo ipasavyo. Halmashauri hizo zimetakiwa kuomba upya mashine
hizo na kuunda vikundi imara baada ya kubainika kuwa vikundi vya awali
vilundwa kisiiasa.
Kikundi cha vijana cha ITIMBA
kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini
kikimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Kasibi
Saguya alipowatembelea ili kujuwa changamoto zinazowakabili. Kikundi
hicho kimeshapata kazi za watu binafsi na shule ili kuwajengea majengo
mbalimbalia na hivyo kupata fedha za kujiendeleza, Halmashauri ya Wilaya
ya Mbeya Vijijini imekubali kuwapa vijana hao ardhi na maeneo ya
kufanyia kazi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bw. James Milanzi akimsikilza Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipofika Ofisini kwake
kukumbusha wajibu wa Halmashauri za Wilaya wa kusaidia vijana ili waweze
kutengeneza matofali ya kujengea nyumba za gharama nafuu na kujipatia
ajira. Halmashauri hiyo imepiga marufuku ukataji miti kwa ajili ya
kuchoma matofali na badala yake wananchi wametakiwa kutumia matofali
rafiki wa mazingira yanayozalishwa kwa kutumia mashine zilizotolewa na
NHC kama msaada kwa vijana katika Halmashauri zote nchini.
Kikundi c ha “CHAPAKAZI”
Wilayani Mbarali kikiwa kinamsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa
NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea kujuwa changamoto
zinazowakabili,Halmashauri ya Mbarali imesaidia vijana vifaa na maeneo
ya kutengenezea matofali hayo na vijana wamehamasika baada ya
kuhakikishiwa soko la tofali zao.
Kikundi cha “JITEGEMEE NA
CALVARY “ Wilayani Tukuyu kikiwa tayari kumsikiliza Meneja wa Huduma
kwa Jamiii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea ili kujuwa
changamoto zinazowakabili, Kikundi hicho kimeishukuru Halmashauri ya
Wilaya ya Tukuyu kwa kuwapa eneo la kufanyia kazi na masoko ya tofali
wanazatengeneza. Kushoto ni Meneja wa NHC Mkoa wa Mbeya Bw. Anthony
Komba.
Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ubisimbali Jesiwande alipokutana
na timu ya NHC na kuchangia hoja ya namna ya kuondoa changamoto za
ajira zinazowakabili vijana nchini, Halmashauri hiyo ambayo vijana wake
hawajafanya vizuri imeapa kuwapa vijana wake mikopo na kuwatafutia
masoko ya matofali yao.
Kikundi cha “Umoja wa
matofali imara” Wilayani Iringa Vijijini ambacho kimeshajenga jengo
kubwa la kibiashara kwa kutumia mashine kilichopewa msaada na NHC
kilipata fursa ya kutembelewa na ujumbe kutoka NHC na kupewa msasa na
hamasa ya kuendelea kujiletea maendeleo kwa kutumia mashine hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa
ya Iringa Bi. Sikitu Mwemsi (kulia) akiomba timu ya NHC iliyofanya
mazungumzo naye Ofisini kwake kuwapa muda badala ya kuwanyang’anya
mashine walizopewa baada ya Halmashauri hiyo kususua kuwasaidia vijana
na kusimamia vikundi vyao, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC ameipa
Halmashauri hiyo mwezi mmoja kujiweka sawa na vijana wake kuanza kutumia
kikamilifu mashine walizopewa msaada na NHC.
Timu ya NHC na Maofisa
Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo ikiwa eneo
linalotumiwa na kikundi cha vijana cha “Muungano Vijana
Kilolo”kilichopewa msaada wa mashine na NHC ambapo walikagua kazi za
vijana hao (hawapo pichani) ambapo Wilaya hiyo imeamua kuwapa mkopo
vijana hao ili wawe na benki kubwa ya matofali.
Kikundi cha vijana cha “Umoja
wa Wafyatua matofali” kilichopo katika Kata ya Mkwawa Manispaa ya
Iringa kikiwa kimeanza kazi ya kutengeneza matofali kilipotembelewa na
timu ya NHC kuona kazi zao. Hiki ni kikundi kinachofanya vizuri katika
Manispaa hiyo yenye vikundi vinne vya vijana waliopewa msaada wa mashine
na NHC za kufyatulia matofali ya kufungamana..
UMOJA WA WAFYATULA
MATOFALI MANISPAA YA IRINGA
Kikundi cha SHIDEPHA ambacho
kilipewa mafunzo ya namna ya kutumia mashine za kutengeneza matofali ya
kufungamana na NHC kikiwa imara na timu ya NHC iliyowatembelea na
kuamua kuwaongezewa uwezo kwa kupewa mafunzo na vifaa vya kufanyia kazi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC baada ya kuona juhudi zao aliamuru
waongezewe mashine mbili ili wasonge mbele na Halmashauri imekitambua
kikundi hicho.
Post a Comment