MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA TANO YA KUHIFADHI QUR-AN TUKUFU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini
wa dini ya Kiislamu wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na
Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu
yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama, iliyofanyika kwenye Msikiti wa
Istiqaam, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheki ya
Sh. Milioni 3, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi
Qur-an Tukufu, Said Nassor Said, aliyehifadhi Juzuu 30, wakati wa hafla
fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi hao wa mashindano
yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Hafla hiyo ilifanyika kwenye
Msikiti wa Istiqaama Ilala jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa
Iran nchini Tanzania, Mehdi Aghajafari, wakati akiondoka kwenye Msikiti
wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi
Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an
Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakati akiondoka kwenye Msikiti wa
Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi
Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an
Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama.
Picha na OMR
Post a Comment